MWALIMU JOYCE APEWA 'WHEELCHAIR' NA HOSPITALI YA MUHIMBILI



Kwa ufupi

Pamoja na hilo hospitali hiyo imejitolea kumpatia huduma ya mazoezi bure ili aweze kutumia kiti hicho  katika shughuli zake za kila siku.

Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili imemkabidhi kiti cha kutembelea (wheelchair) Joyce Kantande ambaye ambaye amepooza.

Pamoja na hilo hospitali hiyo imejitolea kumpatia huduma ya mazoezi bure ili aweze kutumia kiti hicho  katika shughuli zake za kila siku.

MNH imetoa msaada huo baada ya gazeti la Mwananchi kuandika habari kumhusu Kantande iliyomuelezea kuwa licha ya kupooza lakini anamudu kufundisha wanafunzi akiwa kitandani.

Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi Agnes Mtawa amesema uongozi wa Muhimbili uliguswa na habari hiyo ndipo ukaona umpatie msaada huo ambao kwa kiasi fulani utamrahisishia.

Kwa upande wake Kantande amesema; "Nalishukuru gazeti la Mwananchi kwani leo hii naona taratibu ndoto yangu inaanza kutimia kwa miaka 18 nimelala kitandani lakini kwa mazoezi na kiti hiki naamini nitakuwa nimepiga hatua",amesema

0 Comments