MWALIMU RUMANDE KWA AMRI YA MKUU WA WILAYA -HAI

Mkuu wa Wilaya ya Hai, amweka mwalimu rumande kwa kushindwa kujibu swali katika ziara ya kutembelea shule za sekondari,Mkuu wa wilaya ya Hai,Mh.Gelasius Byakanwa alifika shule moja iliyopo ukanda wa chini mwa wilaya ya hiyo akiambatana na afisa elimu msaidizi ndugu Jafari na mwandishi wa habari wa Redio Boma-Hai FM ndugu Davis Minja.

Dc alifanya kikao na walim hao,alianza kwa kuwauliza wangapi wanamfahamu kwa majina,walim walikaa kimya, Dc akawaamuru waandike majina yake kwny karatasi aliyowapa.
Baadhi ya walimu walishindwa na kuwaita WANAFIKI.kosa ni kushindwa kuandika majina yake.

Baada ya mda akawataka waalimu waandike nafasi ya shule mwaka 2015 katika mtihani wa NECTA,mwalim mmoja alishindwa kuandika na alipomfata akimwamuru aandike,mwalim alimjibu hawezi kuandika uongo kwani hakumbiki.Jibu hilo lilimfanya DC apige simu Polisi na kuagiza polisi waje.

Kabla gari la polisi kuja,dc alimwita mwl pembeni na kumwambia achague kati ya kwenda rumande au kupiga push-up 20,lakini mwl alimjibu hawez kupiga push-up kwani anamatatizo ya kiafya.Basi gari lilipokuja mwalim alipandishwa na kupelekwa kituo cha polisi Bomang'ombe.

Dc aliwaambia walimu wakitaka wakashitaki kokote na hata kwny chama chao cha CWT.
Kisha aliwaamuru kupiga picha ya pamoja kama kumbukumbu...

Baada Ya Kikao hicho.
Dc amekuwa aliwapigia sim walim hao na kutaka kujua kinachoendelea.

Taarifa ilifikishwa chama cha walimu CWT-wilaya na kisha kuja kufanya kikao na walimu ilikupata uhalisia wa tukio,ndio mwalim mmoja wa kike kuongeza kuwa baada ya kikao kwisha DC alimpigia simu saa zisizo za kazi ikiwa ni pamoja na usiku akimtala waonane.Mwalim alitoa vielelezo vya sms na muda aliopigiwa (screen shoot) zake na kumkabidhi katibu wa cwt mkoa wa kilimanjaro...

0 Comments