MAHAFALI YA PILI YA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI

Mwenyekiti wa Baraza la Chuko Kikuu cha Ushirika Moshi,Prof Gerald Monela akizungumza wakati wa mahafali ya pili ya chuo hicho yaliyofanyika katika uwanja wa michezo wa chuo .

Makamu wa Mkuu wa Chuo  kikuu cha Ushirika Moshi ,Prof Faustine Bee (Kulia akisoma ujumbe kutoka kwa Kaimu Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.Basil Liheta (kushoto).

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) Spika Mstaafu ,Pius Msekwa akiwapongeza watumishi wa Chuo hicho waliotunukiwa Shahada ya Uzamivu katika vyuo mbalimbali.(P.T)

Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) Prof Faustine Bee akimkaribisha Mkuu wa Chuo hicho,Pius Msekwa kuunda mkusanyiko kuwa Mahafali ya Pili ya Chuo hicho kwa minajili ya kutunukisha vyeti mbalimbali .

Baadhi ya Wahadhiri katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi wakiwa katika Mahafali ya Pili ya chuo hicho yaliyofanyika katika uwanja wa chuo hicho.

“Kwa Mamlaka niliyokabidhiwa ,natangaza mkusanyiko huu kuwa ni Mahafali ya Pili ya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi” haya ni maneno aliyokuwa akiyatoa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi,Pius Msekwa.

Baadhi ya Wahitimu wa Shahada,Stashahada na Astashahada wakihudhurishwa wakati wa mahafali ya pili ya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU).

Wahitimu ya Shahada ya kwanza ya Sheria wakifurahia jambo na Wahadhiri wao (kushoto) Shadrack Madila na George Sizya  katika mahafali hayo.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi,Pius Msekwa akiongoza uongozi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi wakati wa kuhitimisha mahafali ya 2 ya chuo hicho.

Baadhi ya Wageni waalikwa wakitoka katika Mahafali ya Pili ya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.(MoCU).

0 Comments