MAHAFALI YAFANA BAADA YA DR SHIKA KUHUDHURIA

Wahitimu wakiingia ukumbini katika mahafali ya kwanza ya chuo hicho.

Wahitimu wa Chuo cha Sayansi ya Afya wakiingia ukumbini kwa furaha wakiwa na furaha tele.

Wahitimu wakiwa ukumbini

Mkuu wa wilaya akiwa na mkurugenzi wa Chuo hicho pamoja na mke wa mkurugenzi Mrs Bakungile.

Mwanachuo akiendelea kutoa burudani katika uzinduzi wa chuo hicho.

Meza kuu ikifuatilia kwa makini burudani ya nyimbo za asili katika mahafali hayo.

Familia na ndugu wa Mkurugenzi wa Chuo hicho wakiwa katika sherehe hizo wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi

Mkurugenzi wa Chuo cha Sayansi ya Afya Ndugu Yonah Bakungile akitoa neno kwa wahitimu katika mahafali hayo

Wageni waalikwa pamoja na wazazi wakiwa katika sherehe za mahafali na uzinduzi wa chuo cha sayansi ya afya

Mwenyekiti wa bodi ya shule akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Kahama kutoa hotuba yake.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akitoa hutuba kwa wazazi na wahitimu katika mahafali hayo.

Dr. Shika akitoa neno kwenye mahafali hayo

Dr. Shika akishikana mkono na Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu.

Burudani inaendelea

Wahitimu wakiwa wameketi katika nafasi zao 

Mwenyekiti wa mtaa wa Nyasubi Leonard Mayala kulia akiwa na Dr Louis Shika katika sherehe hizo

Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akikakugua maabara ya kufundishia kwa vitendo katika Chuo hicho.

Mkuu wa wilaya ya Kahama akiendelea kupata maelekezo kuhusu elimu ya vitendo wanayoipata wanachuo katika chuo hicho.

Mkuu wa wilaya ya Kahama akiendelea kutembelea vyumba katika chuo hicho.

Mkuu wa wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu amezidua rasmi chuo cha Sayansi ya afya kilichopo Mjini Kahama mkoani Shinyanga ambapo uzinduzi huo umeambatana na mahafali ya kwanza ya wahitimu wa mafunzo hayo katika chuo hicho.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya wilaya ya Kahama akiwemo Mtanzania aliyejizolea umaarufu hivi karibuni Dr. Louis Shika ambaye ameahidi kutoa shilingi bilioni 2 kwa ajili ya kusomesha wanachuo ambao wazazi wao wameshindwa kuwalipia ada na wale ambao ni yatima wazazi wao wamefariki dunia.

Akizungumza katika hahafali hayo yaliyofanyika Novemba 23,2017 Nkurlu aliwataka wahitimu wa fani mbalimbali wilayani Kahama kuwa waadilifu pale wanapopata nafasi ya kuihudumia jamii ili kukidhi matakwa ya kusomea fani hizo.

Nkurulu alisema baadhi ya wahitimu wa mafunzo mbali mbali wamekuwa wakishindwa kukidhi vigezo kutokana na kutokuwa na nia ya dhati ya kutekeleza wajibu wao kwa weledi na uadilifu.

Katika hatua nyingine Nkurlu alimwelezea Dr. Shika kuwa ni mtu wa pekee mwenye utulivu na usikivu na kuongeza kuwa wadau wengine waige kama alichofanya Dr. Shika katika kuinua elimu nchini.

Kivutio kikuu katika sherehe hizo akawa Dr. Louis Shika ambaye hivi karibuni amejingea umaarufu, alipojitokeza katika mnada wa nyumba za kifahari za Bilionea Saidi Lugumi zilizoko jijini Dar es salaam, kupitia msemo wake wa “(900 INAPENDEZA)” ambapo katika mahafali hayo ameahidi kutoa bilioni mbili kila mwaka kusomesha watoto yatima katika wilaya ya Kahama.

0 Comments