Kwa ufupi
Meneja wa Mradi wa Kuboresha Ng’ombe wa Maziwa
Afrika ya Mashariki (EADD II), Mark Txoso alisema hayo alipoutambulisha
mradi huo utakaotekelezwa katika halmashauri tisa za mikoa ya Iringa,
Njombe na Mbeya.
Kila Mtanzania anatakiwa kunywa lita 200
za maziwa na siyo 46 za sasa kwa mwaka mmoja ili kuondoa sumu mwilini na
kujenga afya imara, ilielezwa.
Meneja wa Mradi wa Kuboresha Ng’ombe wa Maziwa
Afrika ya Mashariki (EADD II), Mark Txoso alisema hayo alipoutambulisha
mradi huo utakaotekelezwa katika halmashauri tisa za mikoa ya Iringa,
Njombe na Mbeya.
Mradi huo unakwenda sambamba na mradi kama huo ulioko katika nchi za Kenya na Uganda.
Txoso alisema Mashirika ya Kimataifa ya Chakula na
Kilimo (Fao) na Afya (WHO) yalishaweka viwango vya kila mtu duniani
kunywa walau lita 200 za maziwa kwa mwaka ili kuuweka mwili katika afya
bora, lakini Watanzania wanakunywa kiasi kidogo zaidi cha maziwa
ikilinganishwa na nchi nyingine.
“Watanzania wengi hawanyi maziwa au wanakunywa
kidogo. Hali ni mbaya kwa sababu, wengi hawafikishi lita 200 kwa mwaka
kama ushauri unavyoelekeza,” alisema.
Alisema mradi wa EADD II unalenga kuboresha
ufugaji wa ng’ombe wa maziwa katika Halmashauri za Kilolo, Iringa
Vijijini na Mufindi mkoani Iringa, wakati Halmashauri za Njombe ni
Wanging’ombe, Njombe Vijijini na Njombe Mjini na Mkoa wa Mbeya ni
Rungwe, Mbozi na Mbeya Vijijini.
Alisema mradi utalenga kuboresha mifugo inayotoa
lita 5-7 kufikia lita 18-20 kwa mkupuo na kwamba pia utaboresha malisho
na aina ya ng’ombe.
“Kila halmashauri mkoani humo italazimika kufungua
kituo kimoja cha kushughulikia maziwa na mipango mingine na wafugaji
35,000 wanatarajiwa kuanza katka mradi huo,” alisema.
0 Comments