Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Isaya Mngulu
(kushoto)akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana watu waliokamatwa
na mabomu saba mjini Arusha. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,
Liberatus Sabas.Picha na Filbert Rweyemamu
Kwa ufupi
- Jeshi hilo pia linawashikilia Jeshi
hilo pia linawashikilia watu 25 kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya
milipuko ya mabomu katika nyumba za ibada, mkutano wa hadhara wa
Chadema, mgahawa na nyumba za viongozi wa dini.
Arusha. Jeshi la Polisi
limekamata mabomu saba ya kutupa kwa mkono, risasi sita za bunduki aina
ya Shortgun, mapanga mawili na bisibisi moja, katika operesheni dhidi ya
matukio ya mabomu mjini hapa.Jeshi hilo pia linawashikilia Jeshi hilo pia
linawashikilia watu 25 kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya milipuko
ya mabomu katika nyumba za ibada, mkutano wa hadhara wa Chadema, mgahawa
na nyumba za viongozi wa dini. Mabomu hayo yamekamatwa eneo la
Sombetini nyumbani kwa Yusufu Ali (30) ambaye pamoja na mkewe Sumaiya
Juma (19) wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI),
Isaya Mngulu alisema jana kuwa mabomu sita yaliyokamatwa yametengenezwa
Urusi wakati moja limetengenezwa Ujerumani.“Tunaowashikilia wanatuhumiwa kuhusika na matukio
ya milipuko ya mabomu kuanzia ile ya Kanisa la Olasiti na mengine
yaliyofuata,” alisema Mngulu.Alisema hadi sasa polisi imefanikiwa kubaini
mtandao wa wahusika wa matukio ya mabomu nchini na inawasaka watu
wengine 25 kwa tuhuma za kuhusika na mtandao huo. Licha ya kudai polisi kuwatia mbaroni watu 25,
Mngulu alitaja majina sita pekee wakiwamo walinzi watatu, mmoja wa
Mgahawa wa Vama uliokumbwa na mlipuko wa bomu Julai 7, mwaka huu.“Tunawashikilia walinzi wawili wa Mgahawa Chinese
unaopakana na Mgahawa wa Vama na mwalimu wa Shule ya Msingi Ormet
wilayani Arumeru,” alisema.Polisi pia inamshikilia wakala wa kampuni ya mabasi ambayo haikutajwa, Abdi Salim (31) na mfanyabiashara Said Temba (42).
Kitendawili
Akizungumzia kuhusu mlipuko wa bomu kwenye mkutano
wa Chadema katika Viwanja vya Soweto, DCI alisema hadi sasa hawajabaini
aliyeingiza bomu hilo nchini.“Kiwanda kilichotengeneza bomu lililolipuka kwenye
mkutano wa Chadema Soweto kilishafungwa na hakuna kumbukumbu yoyote
inayoonyesha liliuzwa kwa nani na nchi gani,” alisema Mngulu.Licha ya kukiri kubaini kuwa bomu hilo lilikuwa la
kutengenezwa kiwandani China, polisi haijafanikiwa kujua walioinunua
kutokana na kukosa taarifa muhimu kutoka kwenye kiwanda husika.Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Arusha, Duwan
Nyanda alisema watu 17 wamekamatwa na kushtakiwa kwa matukio ya milipuko
ya mabomu hayo.Alisema watu 16 wameshtakiwa kwa tuhuma za
kuhusika na tukio la bomu kwenye Baa ya Arusha Night Park wakati mmoja
anatuhumiwa kwa bomu la Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi,
eneo la Olasiti.
Kanisa lapiga marufuku vifurushi
Ili kukabiliana na matukio ya kulipuliwa kwa
mabomu, Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha, Parokia ya Bikira Maria
Mama wa Rozari Takatifu ya Mji mdogo wa Mirerani, Simanjiro, Manyara,
imepiga marufuku waumini wake kuingia na vifurushi kanisani.Akizungumza jana kwenye misa iliyofanyika kanisani
hapo, Mwenyekiti wa Parokia hiyo, Benedict Shayo alisema kamati ua
utendaji ya kanisa hilo imeamua hivyo ili kuhakikisha usalama unakuwapo
wakati wa ibada.
0 Comments