
NINA MIEZI MINNE TANGU NIMEAMINIWA NA WANASOMBETINI, TUMEFANYA YAFUATAYO KWA KIFUPI ; (1) Tumepunguza bei ya uzoaji taka toka 2000 na 1500 na sasa wanatoza 1000 ktk makazi. (2) tumejenga madarasa mawili ktk shule ya msingi OSUNYAI na sasa tunaanza ujenzi wa madarasa mengine mawili ktk shule ya msingi SOMBETINI. Pia tunasimamia kikamilifu umaliziaji wa madarasa 8 ya ghorofa ktk sekondari ya SOMBETINI. (3) Tumefanikisha upatikanaji wa mikopo ya jiji kwa vikundi 7 vya kinamama na vijana ambavyo Jana vimepewa jumla ya tsh 13,500,000. (4) Kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii tumewapa kinamama wawili wajane ambao wao ndio ila kitu ktk familia zao yaani bila wao kuhangaika hakuna chakula nyumbani ila mmoja tumempa tsh 100000 kuboresha lolote wafanyalo. (5) BINAFSI TOKA MFUKONI KWANGU nimewapa kinamama watano wanaouza mboga mboga ktk soko la MBAUDA tsh 20000 kila mmoja kuongezea au kufufua mitaji yao, nimtoa jozi 18 za viatu kwa watoto wa aina tofauti ktk kata yangu hasa yatima, nimetoa miti 300 kuboresha mazingira, nimechangia kinamama wa MPARACHICHI VICOBA tsh 350000. (6) naendelea na usimamizi wa ujenzi wa barabara ya lami ya SOKO MJINGA --FFU ambayo inajengwa kwa fedha za ndani za jiji AMBAZO NI USIMAMIZI MAKINI WA CHADEMA KTK KUBORESHA MAPATO YA NDANI YA HALMASHAURI. (7) TUMEFUKUZA MADALALI WOTE WA HUDUMA AMBAO WANAKAA MAENEO YA OFISI YA MTENDAJI. Kuna mengine mazuri yanakuja ktk afya, michezo, vivuko, madawati n.k. NAYAFANYA HAYA KAMA MWANAFAMILIA WA SOMBETINI, KWETU KAZI TU MANENO KWAO!!!!!!!!!!!!!!!
0 Comments