MATOKEO 2014 NI FUNIKA KOMBE...........

Kwa ufupi
Wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka 2014 ndiyo waliohitimu darasa la saba mwaka 2010. Mwaka huo waliofaulu walikuwa 478,912 sawa na asilimia 53.51 ya wanafunzi 895,013 waliofanya mtihani.

Jumamosi iliyopita, Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), lilitangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2014.
Wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka 2014 ndiyo waliohitimu darasa la saba mwaka 2010. Mwaka huo waliofaulu walikuwa 478,912 sawa na asilimia 53.51 ya wanafunzi 895,013 waliofanya mtihani.
Safari yao ya kimasomo imekuwa ikiendelea huku wakiwaacha wenzao njiani, kwani Serikali ikatangaza kuwa wanafunzi 456,350 ndiyo waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2011, ikiwa ni sawa na asilimia 95.3 ya wale waliofaulu mtihani wa darasa la saba.
Hii inamaanisha kuwa waliwaacha wenzao 22,562 ambao hawakuweza kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2011. Wengine wameishia njiani kwani ni wanafunzi 288,365pekee ndio waliofanya mitihani ya kidato cha nne. Wanafunzi 167,985 kati ya 456,350 waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza 2011 walipotelea njiani mpaka sasa. Hii ni idadi kubwa .
Wakati waziri Kawambwa anasoma matokeo yao ya darasa la saba mwaka 2010, alisema walifaulu Kiingereza kwa asilimia 36.47 na Hisabati kwa asilimia 24.70. Hii ndiyo sababu wanafunzi hawa hawakufaulu mtihani wa hesabu kidato cha nne kwakuwa hawakuwa na msingi bora tangu wakiwa shule ya msingi.
Ufaulu wa Hesabu umeshuka hadi asilimia 19.58 tofauti na 24.70 walizopata kwa mtihani wa darasa la saba mwaka 2010. Hata hivyo, inaonekana ufundishaji wa Kiingereza wakiwa sekondari uliimarika kidogo hadi kupata ufaulu wa asilimia 55.10 katika kidato cha nne kutoka asilimia 36.47 za ufaulu wa darasa la saba mwaka 2010.
Mwaka 2014 kulikuwa na vituo vya mitihani 5419 kukiwa na nyongeza ya vituo 1064 ukilinganisha na vituo 4355 vya mwaka 2013. Miaka ya hivi karibuni, baraza limekuwa likitenganisha makundi ya vituo kwa kigezo cha idadi ya watahiniwa.
Lipo kundi la watahiniwa wasiozidi 40 lenye vituo 2,097 na lile la watahiniwa zaidi ya 40 lenye vituo 2,322. Hii inamaanisha kuwa shule za sekondari zimeongezeka zaidi nchini.
Matokeo ya kidato cha nne
Mfumo wa sasa wa ufaulu unatokana na asilimia 30 za maendeleo ya shule na asilimia 70 za mtihani wa mwisho. Hivyo mfumo huu unaonyesha kuwa umechangia kwa kiasi kikubwa aina ya matokeo yaliyotangazwa ya wahitimu wa mwaka 2014. Hebu tuchimbue zaidi tuone kilichopatikana na tufanye tathmini zaidi.
Mwaka 2013, ufaulu ulikuwa kwa asilimia 58.25 yaani wanafunzi 235,227 walifaulu. Kiwango hiki kilijumuisha hata wale waliopata daraja la nne. Lakini wale waliopata daraja la kwanza hadi la tatu walikuwa 74,324 tu, ambao ni sawa na asilimia 21.09. Waliopata daraja la nne walikuwa 126,828 na wahitimu 151,187 walipata daraja sifuri.
Mwaka 2014 wametumia mfumo mpya wa kupanga madaraja kwa njia ya wastani wa ufaulu (GPA). Waliofaulu daraja la kwanza hadi la tatu kwa mfumo huu mpya ni 73,832 sawa na asilimia 30.72. Kati ya hawa, wasichana ni 27,991 na wavulana ni 45,841.
Waliopata sifuri mwaka 2014 ni 72,667 sawa na asilimia 30.24. Hii inaonyesha kuwa kila mwaka kuna ongezeko kubwa la vijana wasioendelea na masomo na wanakuwa sehemu ya jeshi kubwa lisilo na ajira mitaani. Hata hivyo, matokeo haya yanaiumbua Serikali na mpango wake wa Matokeo Makubwa Sasa.
Shule za Serikali
Watanzania wengi waliosoma miaka ya nyuma kuanzia miaka ya 90 na kurudi nyuma watanielewa ninapoongelea shule maarufu za Serikali. Shule hizi zilikuwa na taswira ya kitaifa na zilikuwa zinatoa elimu bora na yenye ushindani sana. Shule hizi ni pamoja na Kibaha, Pugu, Mzumbe, Ilboru, Tabora wavulana wasichana, Msalato, Kilakala, Malangali, Iyunga, Bwiru, Kantalamba, Zanaki, Rugambwa. Matokeo haya yaliyotangazwa yanaonyesha kuwa shule hizi zinazidi kuporomoka.
Shule hizi zote zipo kwenye kundi la watanihiwa zaidi ya 40. Nafasi zao ni kama ifuatavyo : Kibaha ni ya 87, Mzumbe ya 56, Pugu ya 420, Ilboru ya 35, Malangali ya 135, Kilakala ya 96, Msalato ya 71, Tabora Wavulana ya 93 (ingawa inaongoza kwa mkoa wa Tabora), Kazima ya 885, Rugambwa ya 329, Bwiru wavulana ya 234, Zanaki ya 270, Kisutu ya 352, Jangwani ya 243. Ingawa hazijaporomoka kwa kiwango kikubwa lakini ni dalili kuwa ubora wake umeshuka.
Si hivyo tu bali pia shule za kata zina hali mbaya tofauti na Serikali inavyojivunia. Mfano mzuri ni Shule ya Sekondari ya Changanyikeni iliyoko Dar es Salaam ambayo imekuwa ya 2,141 kati ya shule 2,322, na haina kabisa wanafunzi wanaoweza kwenda kidato cha tano.
Shule ya Luana iliyoko mkoani Njombe ni ya 1837 kati ya shule 2097 za watahiniwa chini ya 40. Kibamba ya Dar es Salaam ni ya 1324 kati ya shule 2322. Hata hivyo, zipo zilizofanya vizuri kama vile Makongorosi ya Mbeya, Maria Nyerere ya Njombe na Mwilamvya ya Kigoma.
Sera mpya kuleta ahueni ?
Huenda sera mpya ya elimu ya mwaka 2014 itajibu baadhi ya matatizo ya elimu nchini, lakini bado kunahitajika jitihada za dhati za kuboresha elimu yetu. Wanaonufaika zaidi katika elimu hii ni watoto ambao wazazi wao wanaweza kumudu kuwasomesha katika shule za binafsi ambazo zina ada kubwa na mazingira mazuri ya kujifunzia.
Pia watoto wenye msingi mzuri wa Kiingereza wako katika nafasi nzuri zaidi ya kunufaika na elimu yetu. Itabidi tusubiri utekelezaji wa sera hii mpya ya kufundisha kwa Kiswahili ili hata watoto wale wasioweza kuelewa Kiingereza waweza kuelewa kwa Kiswahili.
Mjadala huu unaweza kuwa mrefu ila nihitimishe kwa kusema kuwa Serikali isipokuwa makini, elimu inayotolewa nchini mwetu itajenga matabaka yatakayozaa chuki kubwa miongoni mwa Watanzania.
Kwa matokeo haya ni watoto wachache kutoka shule za kata watapata fursa ya kuingia kidato cha tano. Na hata wakibahatika kwenda kidato cha tano kuna uwezekano mkubwa wa kushindwa katika mitihani ya kidato cha sita kwakuwa mazingira na msingi wetu wa elimu ni dhaifu.

0 Comments