Waombolezaji wakimfariji mke wa marehemu Kepteni John Komba nyumbani
kwake maeneo ya Tangi Bovu jijini Dar es Salaam.
Kwa ufupi
Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na Hospitali
ya TMJ, ofisi ya Bunge na Chama Cha Mapinduzi na kwamba kwa sasa
taratibu za maziko yake zinaendelea kufanywa .
Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mkurugenzi wa
Kikundi cha Tanzania One Theatre (TOT) Kapteni John Komba amefariki
dunia leo alipokuwa akipelekwa katika hospitali ya TMJ jijini Dar es
Salaam baada ya kuzidiwa.
Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na Hospitali
ya TMJ, ofisi ya Bunge na Chama Cha Mapinduzi na kwamba kwa sasa
taratibu za maziko yake zinaendelea kufanywa .
Aidha taarifa za hivi punde kutoka nyumbani kwake
maeneo ya Mbezi Beach Tangi Bovu zinaeleza kuwa maelfu ya watu kutoka
katika kada mbalimbali wanaendelea kumiminika nyumbani kwa marehemu ili
kutoa faraja kwa familia kwani marehemu ameacha mjane mmoja na watoto
kumi na moja.
Akizungumza na tovuti hii mmoja wa madaktari
aliyempokea wakati anafikishwa hospitali ya TMJ, Dk Elisha Ishan amesema
Komba alifikishwa hospitalini hapo saa 10 jioni leo akiwa mahututi .
"Nilimpokea nilianza moja kwa moja kumpima
shinikizo la damu na vipimo vingine lakini tayari vilikuwa havifanyi
kazi na hapo ndipo tukathibitisha kuwa ndugu yetu ameaga dunia," amesema
Dk Ishan
Pamoja na hayo Dk Ishan amekwepa kutaja moja kwa
moja chanzo cha kifo cha mareheme, hata hivyo amesea Kapteni Komba
alikuwa na tatizo la shinikizo la damu na kwamba siku za karibuni
alifika hospitalini hapo kwenye kiliniki yake ya shinikizo la damu.

0 Comments