Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu vurugu zilizotokea nchini
Afrika ya Kusini jijini Dar es Salaam jana.
Kwa ufupi
Watu hao ambao ndiyo idadi ya Watanzania
waliotambulika kuwa hatarini nchini humo, wanatarajia kuwasili nchini
muda wowote baada ya Serikali ya Afrika Kusini kuridhia. Watakaorejea
nchini ni Watanzania 21, wengine wawili wameomba kuendelea kubaki huko
Dar es Salaam. Watanzania 23
waishio Afrika Kusini wamewekwa kwenye kambi maalumu ya Isipingo nchini
humo ili kupewa ulinzi wa maisha yao yaliyo hatarini kufuatia
mashambulizi yanayofanywa na wazawa dhidi ya wageni.
Watu hao ambao ndiyo idadi ya Watanzania
waliotambulika kuwa hatarini nchini humo, wanatarajia kuwasili nchini
muda wowote baada ya Serikali ya Afrika Kusini kuridhia. Watakaorejea
nchini ni Watanzania 21, wengine wawili wameomba kuendelea kubaki huko.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernard Membe alisema hakuna Mtanzania aliyepoteza maisha
katika vurugu zilizosababishwa na chuki dhidi ya wageni, lakini wapo
Watanzania watatu waliokufa nchini humo kwa sababu nyinginezo.
Membe aliwataja waliofariki kuwa ni Rashid
Jumanne. Alisema Mtanzania huyu alikuwa ni jambazi na aliuawa kilomita
90 kutoka mji wa Durban akiwa kwenye harakati zake za unyang’anyi.
Mtu wa pili alisema anaitwa Athman China. Alisema
kijana huyu aliuawa kwa kuchomwa kisu ndani ya gereza la West Hill.
Membe alifafanua kuwa China alifanya kosa la jinai akafungwa, na huko
gerezani zikatokea fujo za wafungwa. Kijana huyo alikufa baada ya
kuchomwa kisu na wafungwa wenzake.
Ally Mohamed alikuwa ni kijana wa tatu kufa akiwa
Afrika Kusini. Membe alisema Mohamed alikuwa amelazwa hospitali huko
Johanesberg kwa maradhi ya kifua kikuu. Kijana huyo alifariki baada ya
kuugua kwa miezi miwili, na tayari mwili wake umewasili nchini kwa
maziko.
“Kuna habari zimesambaa mitandaoni kwamba
Watanzania wamekufa huko Afrika Kusini. Niweke wazi kuwa hakuna
Mtanzania aliyepoteza maisha kutokana na vitendo vya chuki dhidi ya
wageni. Mpaka sasa ni watu nane tu ndiyo waliopoteza maisha,” alisema
waziri huyo na kuongeza kuwa watu hao wanatoka katika nchi za Ethiopia,
Zimbabwe, Malawi na Swaziland.
Membe alisema aliwasiliana na Waziri wa Usalama wa
Afrika Kusini, David Mahlobo akamthibitishia kuwa hakuna Mtanzania
yoyote aliyekufa. Pia, alimwita balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini
ili aeleze zaidi madhara yaliyojitokeza kwa Watanzania waishio Afrika
Kusini.
0 Comments