Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapambano na Msasani A na B zote za jijini Dar es Salaam leo wamenufaika na mafunzo ya Afya na Usalama barabarani ikiwa ni mwendelezo wa kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahala pa kazi duniani na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na jeshi la Polisi Kanda ya Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo elimu hii pia itaendelea kutolewa katika shule za msingi zingine jijini mapema wiki hii.
Mafunzo hayo yaliyotolewa na wafanyakazi wa kampuni hiyo yalionekana kuwavutia wanafunzi wa shule hiyo ambao pia walishiriki katika mazoezi ya kukabiliana na majanga mbalimbali yanayojitokeza kwa dharura.
Akiongea juu ya mafunzo Mkuu wa Idara ya Afya na Usalama wa Vodacom Tanzania Karen Lwakatare,amesema Vodacom ikiwa ni kampuni inayozingatia usalama wa wafanyakazi wake na watanzania wote kwa ujumla imeamua kutoa mafunzo ya usalama sehemu za kazi kwa wanafunzi ikiamini kuwa wao ndio wafanyakazi wa baadaye ambao ndio tegemeo la kukua kwa uchumi wetu.
“Tumeona pia kuna umuhimu kwa wanafunzi hawa kujua alama mbali mbali za barabarani pamoja na matumizi yake mbali na kuishia kuziona tu kwa macho. Kama suala la usalama barabarani lazima lipewe kipaumbele kwani kama tujuavyo jiji la Dar es Salaam lina changamoto nyingi ukizingatia magari sasa yamekuwa mengi kitu na matumizi ya barabara yanachanganya watu wengi na kusababisha kuwepo na ajali nyingi za barabarani”.Alisema.
0 Comments