YAH: MWALIKO KWENYE KONGAMANO LA WASOMI NA WAFANYABIASHARA
TAREHE 28 MEI 2016 – UKUMBI WA SAFARI HOTEL SAA NANE MCHANA.
Salaam.
Taasisi ya maendeleo ya mkoa wa Arusha(Arusha Development Foundation - ARDF) kwa kushirikiana na ofisi ya MEYA wa JIJI la Arusha na CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO inapenda kukualika kwenye kongamano maalumu litakalowashirikisha wasomi na wafanyabiashara wa mkoa wa Arusha. Kongamano hili litafanyika katika ukumbi wa SAFARI HOTEL, siku ya JUMAMOSI TAREHE 28 Mei 2016 kuanzania SAA NANE MCHANA.
Watoa mada katika Kongamano hili watakuwa ni DR. Vincet Mashinji (Katibu Mkuu – CHADEMA), Profesa Mwesiga Beregu (Mhadhiri wa Chuo KIkuu – SAUT) na Dr. Eliamani Laltaika (Mwanasheria na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Nelson Mandela). Watoa mada wote kwa pamoja watachokoza mjadala wenye kugusa nafasi ya wasomi na wafanyabiashara katika kusababisha na kuchangia ukuaji wa uchumi katika taifa. Mjadala utaangalia mwenendo wa kisera na kimatamko wa awamu hii ya serikali na uhusiano wake na jamii hii ya wasomi na wafanyabiashara katika kuangalia na kujibu swali hili, Je kiuchumi tunakwenda sawa?
Aidha Mstahiki Meya wa JIJI la Arusha kwa Mara ya kwanza, atatoa mada yenye kuanisha na kutoa fursa za kiuwekezaji katika JIJI la Arusha. Sambamba na mada Mstahikim Meya atatoa nyaraka za kuwawezesha wanaotaka kuwekeza katika JIJI la Arusha wazijue fursa na wachukue hatua za kiuwekezaji.
Kongamano hili pia litatoa fursa kwa Mwenyekiti wa MIPANGO MIJI wa JIJI la Arusha kutoa maelezo ya mpango wa JIJI na hatua ambazo zimefikiwa katika kulipanga JIJI hili kuwa la kisasa zaidi lenye kutoa taswira ya makao makuu ya Jumuiya ya Afrika ya MAshariki
Hivyo ukiwa mdau wa muhimu sana wa maendeleo katika nchi hii, nichukue fursa hii kukualika ili uwepo kushiriki katika kongamano hili la kipekee na la aina yake.
0 Comments