Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
amemuapisha Bw. Oliva Paul Joseph Mhaiki kuwa Mwenyekiti wa Tume ya
Utumishi wa Walimu (TSC).
Aidha, Rais Magufuli amemuapisha Mwl. Winifrida Gaspar Rutaindurwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC).
Rais Magufuli alifanya uteuzi wa Mwenyekiti na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu tarehe 15 Julai, 2016.
Viongozi
hawa wanakuwa wa kwanza kuongoza Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) tangu
Tume hiyo ilipoundwa kwa mujibu wa sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu
Namba 25 ya mwaka 2015 ikiwa na majukumu ya kusimamia na kuratibu
masuala yanayohusu utumishi wa walimu.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
27 Julai, 2016
0 Comments