MEYA WA JIJI LA ARUSHA- CHADEMA KUGAWA ZAIDI YA MILIONI 400 KWA WAJASIRIAMALI LEO

Halmashauri ya Jiji la Arusha ambayo inayoongozwa chama Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) leo itagawa zaidi ya milioni 400 kwa vikundi 96 vya ujasiriamali kutoka katika kata 25 ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi

Zoezi hili ni la awamu ya kwanza, na linafanyika kwa mara ya kwanza katika historia ya Halmashauri ya Arusha Mjini. Haijawahi kufanyika katika kipindi chote cha uongozi wa CCM zaidi ya miaka 50 iliyopita, ambapo wamekuwa wakizitumia kwa matumizi wanayojua wenyewe  badala ya walengwa.

Katika hafla hiyo ya makabidhiano ya hundi mikopo hiyo nafuu kwa umma wa Arusha Mjini, itafanyikia katika ukumbi wa Azimio kuanzia saa  tano asubuhi.

Mh Meya wa Jiji Kalisti Lazaro ndiye atakayesimamia zoezi hili kama Meya wa Jiji linaloongozwa na Chadema akiataambatana Mkurugenzi, na maofisa wengine wa Jiji.

Meya Kalisti amesema zoezi hili ni endelevu na Halmashauri yake  itahakikisha lengo kuu la kuwatumikia wananchi na kuinua hali  zao za kimaisha linatimia kama walivyoahidi sambamba na kuhakikisha kero za msingi  kama maji, huduma za afya,barabara  na umeme  zinamalizwa kabisa.

Mh Kalist aliongeza kuwa baada ya halmashauri kuchukuliwa na chadema taratibu zote ziliwekwa wazi, ambapo kwanza kama Halmashauri yeye na Madiwani wake walianza kuthibiti ubadhirifu na kuziba mianya ya ukwepaji kodi na wizi, kiasi cha kupandisha makusanyo ya fedha kutoka Milioni 300 kwa mwezi hadi Bilioni 1.2 kwa mwezi.

Mh Kalist alisema kuwa alishirikiana na Madiwani kuhakikisha vikundi vingi vinasajiliwa hasa makundi ya vijana na akina mama ili waweze kupata mikopo ya kujikwamua kiuchumi.  Amesema kuwa taratibu za ugawaji mikopo upo wazi hakuna urasimu wala ukada wa kisiasa kama ilivyokuwa huko nyuma Halmashauri ikiongozwa na maccm.

Mh Kalist amesisitiza kuwa Halmashauri itakuwa ikiendelea kutoa mikopo kila baada ya miezi mitatu kwa vikundi na kuhakikisha wananchi wanafurahia utendaji kazi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha

0 Comments