UFISADI WA UJENZI WA CHOO - JIJI LA ARUSHA

Meya Jiji LA Arusha ashtukia Ufisadi ujenzi wa matundu mawili ya choo kwa mil.12

Mstahiki meya Jiji LA Arusha Kalist Lazaro ameshtukia harufu ya ufisadi kwenye ujenzi wa matundu mawili ya Choo cha zahanati ya Elerai.

Mstahiki meya akiwa pamoja na madiwani wakikagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayojengwa kwa fedha za halmashauri ya Jiji kama sehemu ya utekelezaji wa ahadi za halmashauri kwa wananchi wa Jiji la Arusha, alisema haiingii kilini kuwa matundu mawili ya Choo tens madogo kuigharimu halmashauri fedha nyingi kiasi hiki. 

Mstahiki Meya amesema hawezi kupokea taarifa ya gharama za ujenzi wa Choo hicho hadi hapo atakapojiridhisha baada ya vyombo vyenye mamlaka husika kufanya uchunguzi. Amesema kuwa Watu wa Arusha walituamini ili tuweze kusimamia rasilimali zao kwa uwazi na ukweli, na kwamba hayuko tayari kuona Watu wachache wenye tamaa wakijinufaisha kwa kodi za wananchi.

Mstahiki Meya ameahidi kulifuatilia ili kubaini ukweli inakuwaje matundu mawili ya Choo yagharimu kiasi cha Fedha halali kwa Malipo ya Tsh. Milioni 12.

Mmoja wa Mtumishi wa Halmashauri alipoulizwa kuhusu harufu ya ufisadi kwenye Choo hicho hakuwa tayari kuzungumza zaidi ya kusema "Haya ndiyo madhara ya Madc kuingilia majukumu ya halmashauri kinyume na utaratibu angalieni wanaleta Watu wa namna gani sasa"

0 Comments