Kwa nafasi yangu kama Meya wa Jiji la Arusha napenda kutoa taarifa juu ya masuala matatu ya msingi ambayo ni:
Umuhimu wa Elimu Utii wa maadili ya viongozi wa umma na
Mipaka ya uongozi katika utumishi wa umma.
Katika muktadha wa ungozi wa mkoa na jiji letu la Arusha.
Umuhimu wa Elimu
Maendeleo ya nchi yeyote yanatagemea ubora wa elimu wanayopata watoto wa nchi hiyo, na kwa kuzingatia msingi huo muhimu Taifa letu limetunga sheria na taratibu mbalimbali zinazoongoza utoaji wa elimu katika nchi yetu. Na kwa Tanzania sheria inayoongoza utoaji wa elimu ya msingi ni The Primary School Compusory Attendance Act, sheria inayolazimu wanafunzi, wazazi, walimu na wadau wote wa elimu kuhakikisha kwamba wanafunzi wa shule ya msingi wanafika shule na kupata elimu bila kukosa katika siku zote zilizopagwa kwa mujibu wa Wizara ya Elimu.
Kwa mujibu wa Sheria hiyo ni marafuku, na ni kosa kwa mtu yeyote kumkosesha mwanafunzi wa shule ya msingi masomo yake.
Pamoja kuwepo kwa masharti hayo ya kisheria Mkuu wa mkoa wa Arusha siku ya jana tarehe 19 September 2016 amefunga shule zote kwa siku nzima kinyume cha Sheria, kwa kisingizio cha kukutana na walimu wa shule hizo. Takribani shule 48 zimefungwa na kufanya wanafunzi Zaidi ya thelathini elfu (30,000/-) kukosa masomo na kuharibu ratiba iliyowekwa na wizara ya elimu.
Mkuu wa mkoa ni mteule wa Rais, mteule wa Rais anapovunja sheria wazi wazi ni dhahiri kwamba utawala huu auheshimu utawala wa sheria.
Ni muhimu kufahamu pia kwamba athari za kukosa shule kwa siku nzima kwa wanafunzi wa shule za msingi haziwezi kurekebika. Kwa kawaida siku moja ya shule inakua na vipindi Zaidi ya vitano (5) ambavyo kwa siku ya jana walivikosa vyote.
Walimu wa kuu wa shule za msingi wamelalamikia kitendo cha wanafunzi kukosa masomo kwa siku ya jana kwa kuzingatia kuwa wamepewa malengo ya kuyatimiza kwa kufaulisha wanafunzi na wizara.
Wazazi wamepata wakati mgumu kwa watoto wao kurudishwa nyumbani bila taarifa kwa siku ya jana, izingatiwe kuwa wazazi hawakuwa na ratiba ya kuwapokea watoto wao asubuhi ya jana.
Dhana ya Elimu bure imekiukwa na imeathirika kwani kodi za wananchi zimepotea kwa siku nzima ya jana kwa wanafunzi kukosa masomo.
Kwa nafasi yangu kama meya ninawasiliana na Rais Magufuli, na Wizara ya Elimu kuona ni hatua gani Rais na Wizara inachukua dhidi ya mkuu wa mkoa na Mkurugenzi wa Jiji na wadau wote waliosababisha hasara hii, na hujuma dhidi ya Serikali inayojitahidi kutengeneza madawati na kusaidia kutoa elimu bure nchini.
Utii wa maadili wa viongozi wa umma
Sheria ya maadili ya viongozi wa umma inawataka viongozi wote wa umma, na katika muktadha wa Jiji la Arusha, sheria inatutaka Madiwani, Meya, Mbunge, Mkuu wa Mkoa, na viongozi wengine wakuteuliwa na kuchaguliwa kuheshimu Miiko na Maadili ya Viongozi wa Umma.
Viongozi wanapaswa kuwa wakweli, wawazi, waadilifu na wenye kuheshimu sheria.
Mosi, Katika hali ya isiyotarajiwa na inayokiuka sheria ya maadili ya utumishi wa umma, Mkuu wa Mkoa wa Arusha amewadanganya watumishi wa kada ya chini ya umma ambapo ni waalimu pale alipowahidi kwamba atawalipa walimu malimbikozo ya kwa makusanyo ya makato ya madiwani.
Mkuu wa mkoa anajua fika kwamba mishaara na stahiki za waalimu zinalipwa na Serikali Kuu kupitia Wizara ya Utumishi na sio halmashauri, hivyo kumuagiza Mkurugenzi wa almashauri wa Jiji la Arusha kuwalipa walimu malimbikizo hayo ni udanganyifu zidi ya watumishi hawa muhimu, na ukuhukwaji wa wazi wa Maadili ya viongozi.
Pili, Mkuu wa Mkoa na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha wamekua wakiupotosha umma juu ya suala la posho za madiwani wa Arusha.\
Ifahamike kuwa Sera ya CHADEMA ambayo ndio inayoongoza halmashauri ya Arusha ni kuwa posho zote za vikao(sitting Allowances) zifutwe na badala yake mishaara na maslahi ya wafanyakazi yaboreshwe Ili kuongeza ufanisi.
Anachokiita Mkuu wa Mkoa wa Arusha kama posho tulizojiongezea madiwani wa Arusha ni jambo ambalo halijui kwa uwelewa wake finyu wa masuala ya utawala wa fedha za halmashauri, au makusudi yake yenye nia ya kuichafua halamshauri hii inayoongozwa na CHADEMA.
Pesa ambazo madiwani tumekuwa tukilipwa kama posho ziliamuliwa mwaka 2008 June, tarehe 10 wakati ambao Halmashauri hii ilikuwa ikiongozwa na Meya Laurance Heddi, Mbunge akiwa Felix Mrema wote wa CCM na Kamati ya Fedha ilikuwa inaongozwa na marehemu Jubilate Kilewo ambae pia alikuwa mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Arusha.
Hivyo kinachoendelea leo ni utekelezaji tu maamuzi wa Chama cha Mkuu wa Mkoa, na kama Mkuu wa Mkoa anafikiri kwamba maamuzi hayo hayakuwa sahihi anatakiwa kufanya maamzu yake kwa mujibu wa sheria ya uthibiti wa fedha za halmashauri imetolewa na waziri na kutolewa na mpiga chapa wa serikali kupitia - the Local Authority Financial Memorandum ya mwaka 2011.
Ambapo kanuni hizi zinataka awajibishwe yule aliyeamua pesa hizi kulipwa, na sio mlipwaji.
*Kutokana na ukiukwaji huu wa wazi mimi pamoja na madiwani wenzangu tumeamua kumshitaki mkuu wa mkoa wa Arusha kwenye Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, na Kwenye Mahakama zetu nchini ili kudhihirisha kwamba CHADEMA tunasimamia utawala wa Sheria katika nchi yetu*
*Wanasheria wetu wanaandaa mashtaka mahakamani ni dhidi ya Athuman Kihamia yeye binafsi na si Mkurugenzi wa jiji*
Mipaka ya Uongozi katika Utumishi
Uongozi wa nchi yetu unapatikana kwa mujibu wa sheria. Na viongozi wanaopewa mmlaka kwa mujibu wa sheria wanawekewa mipaka na masharti ya mamlaka yao na sheria.
Wakuu wa mikoa wote nchini wanapatikana na kuongozwa na Sheria ya Tawala za Mikoa mwaka 1997, kwa mujibu wa sheria hii mkuu wa mkoa wowote ana majukumu mawili tu;
Kuongoza kikao cha ulinzi na usalama na kusimamia ulinzi na usalama wa mkoa
Kuwezesha utekelezaji wa maazimio na maamuzi ya halmashauri zilizopo kwenye mkoa wake.
Na hakuna jukumu linguine lolote.
Hivyo ni muhimu wananchi kufahamu kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha hana majukumu anayojipa ya ukaguzi, usimamizi wa elimu nakadhalika.Pia kif.6 1 R.adm.ACT 1997,-{THE PRESIDENT MAY BY WRITING UNDER HIS HAND AND THE PUBLIC SEAL,DELEGATE ANY OF HIS FUCTIONS AND DUTIES UNDER ANY WRITTEN LAW TO ANY REGIONAL COMMISSIONER)
-Mkuu wa mkoa hana mamlaka kufunga shule au kuahirisha masomo ya mwanafunzi wa nchii
-Mkuu wa mkoa hana mamlaka ya kuwa mhasibu wa halmashauri wala mkaguzi wa halmashauri
-Mkuu wa mkoa hana mamlaka ya kupanga au kuamua matumizi ya halmashauri yeyote.
-Mkuu wa mkoa hana mamlaka ya kuagiza mkurugenzi namna pesa za halmashauri inatumikaje.
Kumbuka nchi hii uchaguzi ulifanyika kwa watu wa tatu tuu –Rais ,mbunge na madiwani .Sanduku la mkuu wa mkoa halikuwepo kwenye uchaguzi ,hivyo hapaswi kujiita mwakilishi wa Rais kila mahali.Tuna Rais mmoja tu,na hakuna Rais anatoa mamalka yake hovyo hovyo kwa watu wa aina hii na hata hivyo Rais mwenyewe hana mamlaka ya kufunga shule ILA waziri husika wa Elimu*
Imetolewa leo 20.09.2016
Kalist Lazaro
Mstahiki Meya
Jiji la Arusha
0 Comments