Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi.
Kwa ufupi
Watoto 25 kati ya 70 wamefanyiwa upasuaji huo ambao umefanikiwa kwa kwa asilimia 100.
Dar es Salaam. Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka Italia, Grace Parker amesema waliofanyiwa upasuaji katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wanaendelea vizuri na baada ya siku chache wataruhusiwa.
Watoto 25 kati ya 70 wamefanyiwa upasuaji huo ambao umefanikiwa kwa kwa asilimia 100.
Watoto hao wamefanyiwa upasuaji na jopo la madaktari bingwa wa moyo kutoka Taasisi ya Kids Mendig Organisation ya Marekani.
Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi amesema upasuaji huo ulianza Septemba 9 na unatarajia kumalizika Septemba 19.
“Tumewafanyia upasuaji watoto 25, kumi na moja ni wa upasuaji wa kufungua kifua. Mbali na watoto wa Tanzania, tumepokea watatu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na wawili Uganda,” amesema.
Profesa Janabi amesema inaonyesha kwambha taasisi hiyo imeanza kuaminiwa kwa matibabu hayo ambayo kwa Bara la Afrika yanapatika nchini Tanzania na siyo lazima kwenda nje ya bara hili.
0 Comments