Akithibitisha kuhusu ajali hiyo msemaji wa wizara hiyo, Nsachris Mwamwaja amesema ajali hiyo imetokea asubuhi Chalinze mkoani Pwani.
Dar es Salaam. Ajali ya gari iliyotokea leo asubuhi imesababisha kifo cha Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya Afya kwa Umma wa Wizara ya Afya, Maendekleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hellen Semi.
Akithibitisha kuhusu ajali hiyo msemaji wa wizara hiyo, Nsachris Mwamwaja amesema ajali hiyo imetokea asubuhi Chalinze mkoani Pwani.
Amesema pia katika ajali hiyo, mkurugenzi wa huduma za kinga wa wizara hiyo, Dk Neema Rusibamayila amejeruhiwa.
Amesema maofisa hao walikuwa wanakwenda mkoani Dodoma kuhudhuria mkutano wa waganga wa mikoa unaoanza kesho.
0 Comments