HONGERENI SANA MOI

Kwa Ufupi

Upasuaji huo ambao umefanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini ulitumia   teknolojia ijulikanayo kama 'Posterior Instrumentation and Fusion' ambayo inahusisha uwekaji wa vyuma maalum kwenye mfupa wa mgongo katika sehemu ya juu na chini ya mfupa wa mgongo na kuufanya mgongo unyooke.

Dar es Salaam. Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa mara ya kwanza imefanya upasuaji mkubwa wa kunyoosha mfupa wa mgongo wa mtoto uliopinda (kibiongo) kitaalam unafahamika kama ‘Scoliosis’.

Upasuaji huo ambao umefanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini ulitumia   teknolojia ijulikanayo kama 'Posterior Instrumentation and Fusion' ambayo inahusisha uwekaji wa vyuma maalum kwenye mfupa wa mgongo katika sehemu ya juu na chini ya mfupa wa mgongo na kuufanya mgongo unyooke.

MOI imefanikiwa kufanya upasuaji huo kupitia madaktari bingwa walioko kwenye mafunzo ya ubobezi wa juu katika upasuaji wa Mifupa na mgongo kwa watoto kwa kushirikiana na madaktari bingwa kutoka Marekani.

Akizungumza leo Kaimu Mkurugenzi wa MOI Dk Othman Kiloloma, alisema uanzishwaji wa upasuaji huo umetokana na kuanzishwa kwa ushirikiano wa kimafunzo kati ya taasisi ya MOI na Chuo Kikuu cha madaktari bingwa wa upasuaji cha Afrika Mashariki, Kati na Kusini COSECSA na madaktari bingwa kutoka Marekani.

0 Comments