Wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartered wakiongoza matembezi ya kuadhimisha siku ya macho duniani kwa lengo la kuwasaidia wenye uono hafifu kupata matibabu na miwani bure. Picha na Muyonga Jumanne
Kwa Ufupi
Hayo yameelezwa leo (Alhamisi) katika maadhimisho ya Siku ya Macho Duniani, yenye kauli mbiu 'Huduma ya macho kwa wote' yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini hapa.
Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa zaidi ya Watanzania 700,000 wana matatizo ya macho, huku wengi wao wakisumbuliwa na tatizo la presha ya macho.
Hayo yameelezwa leo (Alhamisi) katika maadhimisho ya Siku ya Macho Duniani, yenye kauli mbiu 'Huduma ya macho kwa wote' yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini hapa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi amesema tatizo la macho ni kubwa kwa sababu mpaka sasa hospitali hiyo imehudumia jumla ya wagonjwa 87,000.
"Tunahudumia wagonjwa wengi na wiki hii ya macho pekee. Hadi sasa tumehudumi wagonjwa 400," amesema Msangi.
0 Comments