MFUMUKO WA BEI WASHUKA

Kwa ufupi

Akitoa takwimu hizo, mkurugenzi wa sensa na takwimu za jamii, Ephraim Kwesigabo amesema kupungua huko kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula.

Dar es Salaam. Mfumuko wa bei wa Taifa wa Septemba, mwaka huu umepungua mpaka kufikia asilimia 4.5 kutoka 4.9 iliyokuwa Agosti.

Akitoa takwimu hizo, mkurugenzi wa sensa na takwimu za jamii, Ephraim Kwesigabo amesema kupungua huko kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula.

Amesema bidhaa za chakula zilizopungua bei ni samaki, dagaa na viazi vitamu. Kwa upande wa bidhaa zisizo za chakula, ametaja gesi, petroli na dizeli.

"Uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia Sh97.04 kwa Septemba mwaka huu kutoka Desemba, 2015 ikilinganishwa na Sh96.83 iliyokuwa Agosti, 2016," amesema mkurugenzi huyo.

0 Comments