MWALIMU MWINGINE ADHALILISHWA, SERIKALI KIMYA


Mkurugenzi halmashauri ya wilaya Misungwi amemdhalilisha mwalimu wa shule ya sekondari Shilala iliyopo wilayani humo baada ya kumuamrisha kudeki darasa huku wanafunzi wake wakimshuhudia

Tukio hilo lilitokea pale ambapo mkurugenzi huyo akiwa ameambatana na baadhi ya mafisa walipo fika shuleni hapo mida ya jioni, muda ambao wanafunzi wa kidato cha nne walikuwa wakijisomea ili kujiandaa na mitihani.

Inasemekana Mkurugenzi alipofika sekondari hiyo ya Shilala alitembelea madarasa baadhi na kukuta darasa moja likiwa chafu, ndipo akamuhitaji mwalimu aliye karibu kuja kujibu kwa nini darasa chafu na baada ya hapo mkurugenzi huyo akamwamrisha mwalimu huyo kudeki darasa hilo jambo ambalo mwalimu huyo hakuwa na pingamizi ingawa mwanzo alidhani huenda anaambiwa awaambie watoto wasafishe hivyo akawa anafanya mpango wa kuwaambia wanafuzi.

Katika hali isiyoyakawaida Mkurugenzi bila hata chembe ya busara akamwambia mwalimu udeki wewe mwenyewe, mwalimu hakuwa na ajizi akatafuta ndoo na maji na kuanza kudeki huku wanafunzi wakimshuhudia.

Kwa maoni yangu kama mwalimu nilitarajia jambo hili na tukio alilofanyiwa mwalimu Batuli wa shule ya msingi Ungalimited Arusha yangechukuliwa kwa uzito kama lile la sekondari ya Mbeya ingeleta haueni kwa hadhi ya waalimu Tanzania

Kimsingi anapodhalilishwa mwalimu mmoja na serikali ikachelewa kuchukua hatua watakaoathirika ni wanafunzi na ubaya wa athari za kielimu uchukua muda kabla ya kugundulika na ikigundulika hakuna ushaidi wa moja kwa moja wa malipizi ya waalimu kwa wanafunzi.

Serikali isisababishe waalimu uchukia ualimu na ufundishaji kwakuwa madhara yake ni makubwa kwa vizazi vijavyo.

0 Comments