UN kusomesha vijana 50,000
Kwa ufupi
Akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 71 ya UN Mratibu Mkazi wa umoja huo Alvaro Rodriguez alisema hatua hiyo ni endelevu kwani tayari vijana 10,000 wamewezeshwa kutambua malengo hayo hivyo itasaidia kuleta mabadiliko ya kiuchumi nchini.
Dar es Salaam. Umoja wa Mataifa (UN), umejipanga kushirikiana na wadau wake kuwaelimisha vijana 50,000 hapa nchini ifikapo mwaka 2017.
Akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 71 ya UN Mratibu Mkazi wa umoja huo Alvaro Rodriguez alisema hatua hiyo ni endelevu kwani tayari vijana 10,000 wamewezeshwa kutambua malengo hayo hivyo itasaidia kuleta mabadiliko ya kiuchumi nchini.
"Tanzania ina changamoto kadhaa ikiwamo ya ongezeko la vijana na mahitaji yao tunahitaji kuhakikisha kwamba vijana nchini wanawajibika, katika kuejiendeleza na kuendeleza taifa ili kupata maendeleo chanya katika maisha yao.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Waziri na Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Agustino Mahiga alisema UN imekuwa ikishirikia vyema na Tanzania kwa mambo mengi ya maendeleo, ulinzi na Usalama.
Alisema UN imekuwa ikiitumia wanajeshi wa nchi nyingi ikiwamo Tanzania katika kulinda amani kwenye nchi zilizopo kwenye migogoro, hatua ambayo imekuwa ikisaidia vijana kupata ajira na ujuzi wa masuala ya kiusalama.
0 Comments