Kwa Ufupi
Mhifadhi Mkuu wa hifadhi hiyo, Dk Fredy Manongi alitoa taarifa hiyo jana kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo katika kikao cha wajumbe wa baraza la wafugaji, viongozi wa serikali na watendaji wa NCAA.
Ngorongoro.Watu wawili wamefariki duniani na wengine wanane wamelazwa katika hospitali ya Enduleni ndani ya Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa ugonjwa wa sotoka.
Mhifadhi Mkuu wa hifadhi hiyo, Dk Fredy Manongi alitoa taarifa hiyo jana kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo katika kikao cha wajumbe wa baraza la wafugaji, viongozi wa serikali na watendaji wa NCAA.
Dk Manongi alisema ugonjwa huo unaotokana na kula nyama ya mifugo, ambaye tayari ameathirika, umelikumba eneo la Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kutokana na idadi kubwa ya mifugo iliyoingizwa katika hifadhi hiyo.
0 Comments