UZEE HAKUNA WAKUUKWEPA- BAZECHA

Katika kuadhimisha Siku ya Wazee Duniani tarehe 1/10 kila mwaka, kwa mwaka huu Chadema Kanda ya Kaskazini imefanya kongamano la wazee bila kujali itikadi zao  walijumuika ili kupata fursa ya kupaza sauti yao kwa Mheshimiwa Rais kuwakumbuka katika maswala na madhila kadhaa yanayowakabili.

Katika kongamano hili Mgeni Rasmi alikuwa Mhe. Hashim Issa Mwenyekiti wa Baraza la wazee wa Chadema Taifa (BAZECHA) na kabla ya mgeni rasmi kuhudhuria kongamano alitembelea vituo vya kuhudumia wazee ili kupata wasaa wakuzungumza nao na kuwashika mkono.

Akizungumza na baadhi ya wazee kata ya Ungalimited amewaambia wazee wasivunjike moyo kwa kutopewa fursa ya kushauri wala kushiriki mabadiliko katika serikali, " tushikamane na kupaza sauti yetu kwani uchumi tuliujenga wakati wa ujana wetu hivyo tukumbushe mara kwa mara kuwa sisi ni sehemu ya mafanikio yaliyoko sasa" alisema Mh Hashimu Issa

Pia katika kongamano hili Mstahiki Meya Kalist Kalisti Lazaro katika hotuba yake aliwahaidi wazee kuwa Halmashauri yake imewapa kipaumbele hasa katika huduma ya afya kwa kuwa na dirisha maalumu ya kuwahudumia bure, pia wanaendelea na mkakati wakuwaondoa kwenye kodi za majengo au nyumba wanazoishi.

Kongamano hili ni la kwanza kuwahi kufanyika iliongozwa na Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini Mh  Amani Golugwa nae katika hotuba yake  alisisitiza kuwa katika Halmashauri zinazoongozwa na Chadema kanda ya Kaskazini wamekubaliana  kuwasaidia kwa vitendo kwakuwa wamebaini serikali kushindwa kutekeleza ahadi zao kwa wazee. " Tumekubaliana kuwasaidia kwa vitendo katika afya, uchumi wenu na kuwapigania kupata pensheni bila kujali mliajiriwa ama la" alisema Mh Amani Golugwa

Kwa kuthibitisha vitendo alitoa zawadi ya Vitenge kwa baadhi ya wazee wanawake kwa kutamvua kuwajibikaji kwa  weledi wa hali yajuu kunakofanywa na wazee wanawake yaani bibi zetu kama taifa.

Katika kuhitimisha kongamano wazee waliohuduria walipewa fursa ya kutoa maoni yao kwa serikali ila mgeni rasmi afikishe kwa Mhe. Rais John Pombe Magufuli.

Baadhi ya wazee waliopata nafasi ya kuongea walisisitiza kuwa wao ni Tunu na Hazina ya taifa hivyo wahusishwe kwenye maamuzi ya nchi, waliendelea kusema wasibaguliwe kwa namna yoyote, wapewe stahiki yao ya kuhusishwa na kuhudumiwa kiafya na pensheni.

Wamesema kuwa wanaposhauri serikali isiwapuuze kwakuwa wanauzoefu wa kutumikia taifa hivyo ni haki yao kutoa maoni na kufanyiwa kazi na serikali waliyoiweka madarakani.

Walimalizia kwa kauli yao ya "Uzee... Hakuna wa kuukwepa"

0 Comments