WALIMU WAIDAI SERIKALI SH 273 MILIONI

Walimu waidai Sh273 milioni

Kwa Ufupi

Akizungumnza wakati wa sherehe ya kukabidhi mabati kwa walimu sita waliostaafu hivi karibuni kama mkono wa kwa heri ambao kila mmoja alikabidhiwa mabati 20, Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wilayani hapa, Aidan Mahelela alizitaja idara zinazodai kuwa ni Elimu ya Msingi Sh118,623,752, Sekondari Sh 126,612,507, Ukaguzi Sh12,784,610 na Chuo cha Ualimu Nachingwea walimu wake wanadai Sh14,766,980.

Nachingwea. Walimu wilayani  hapa Mkoa wa Lindi, wanaidai Serikali Sh272.8 milioni za malimbikizo ya mishahara, likizo, masomo na uhamisho, huku walimu wastaafu 26 wakiwa hawajalipwa mafao yao kati ya Aprili na Julai, mwaka huu.

Akizungumnza wakati wa sherehe ya kukabidhi mabati kwa walimu sita waliostaafu hivi karibuni kama mkono wa kwa heri ambao kila mmoja alikabidhiwa mabati 20, Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wilayani hapa, Aidan Mahelela alizitaja idara zinazodai kuwa ni Elimu ya Msingi Sh118,623,752, Sekondari Sh 126,612,507, Ukaguzi Sh12,784,610 na Chuo cha Ualimu Nachingwea walimu wake wanadai Sh14,766,980.

Mahelela alizitaja taasisi za Serikali  zinazodaiwa  kuwa ni Mkurungezi Mtendaji  wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, ofisi ya Katibu Mkuu wa Tamisemi na ofisi ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi.

Alisema licha ya madai ya Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako kudai kuwa walimu wote nchini walilipwa madai yao yote, Nachingwea hawana taarifa wala hakuna aliyelipwa.

0 Comments