Mwigulu aagiza askari wanaodai mishahara tangu Agosti kulipwa
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba
Kwa ufupi
Nchemba amesema hayo leo alipofanya mkutano na maafisa wa uhamiaji makao makuu na kuwataka watumishi wanaohusika na mishahara kufika kesho saa 2:00 asubuhi ofisini kwake kutoa maelezo juu ya suala hilo ili kuondoa mkanganyiko wa taarifa uliopo.
Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameagiza watumishi wanaohusika na suala la mishahara ya askari 291 wanaodai hawajalipwa tangu kuajiriwa Agosti mwaka huu wawalipe haraka.
Nchemba amesema hayo leo alipofanya mkutano na maafisa wa uhamiaji makao makuu na kuwataka watumishi wanaohusika na mishahara kufika kesho saa 2:00 asubuhi ofisini kwake kutoa maelezo juu ya suala hilo ili kuondoa mkanganyiko wa taarifa uliopo.
"Kila mahala wanakupa sababu zao, wengine wanasema kuna makosa ya herufi, wengine tarehe za kuzaliwa ila siamini kama uhakiki wa majina hayo unachukua muda wa miezi minne, wapeni askari hao stahiki zao," amesema Nchemba.
Mwananchi
0 Comments