BILIONI 690 SERIKALI ITATOA WAPI? - MH MBOWE

Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe

Kwa ufupi

Wawili hao walirushiana vijembe jana akianza Mbowe ambaye aliishutumu Serikali akisema haiwezi kuwa na miujiza ya kupeleka fedha hizo huku akihoji yalikoishia mabilioni ya JK.

Dodoma. Mpango wa Serikali wa kupeleka Sh50 milioni kwa kila kijiji umeibua malumbano na majibizano ya kisiasa ndani ya Bunge kutoka kwa kiongozi wa Upinzani Bungeni Freeman Mbowe na Waziri wa Kazi, Sera, Uratibu na Bunge,  Jenister Mhagama.

Wawili hao walirushiana vijembe jana akianza Mbowe ambaye aliishutumu Serikali akisema haiwezi kuwa na miujiza ya kupeleka fedha hizo huku akihoji yalikoishia mabilioni ya JK.

“Ni miujiza gani ambayo Serikali itatumia kufikisha Sh50 milioni kwa kila kijiji ikiwa fedha za mikopo ya wanafunzi mmeshindwa kulipa na katika mpango huo zinatakiwa Sh690 bilioni na tunajua kuwa kuwa Serikali imefilisika,” alihoji Mbowe.

Waziri Mhagama alikanusha Serikali kufilisika badala yake akasema ni mipango tu na kuwa wakati wowote baraza la mawaziri litakutana na kupitisha mpango huo.

0 Comments