Kwa ufupi
Mkutano huo, unatarajiwa kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), kwa kushirikisha taasisi za fedha nchini na wadau wengine kutoka mashirika ya umma.
Arusha. Mkutano mkuu wa mwaka wa taasisi za fedha nchini ulioandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), unatarajiwa kufanyika kwa siku mbili jijini hapa ambapo pamoja mambo mengine inaelezwa utajadili hali ya kiuchumi nchini.
Mkutano huo, unatarajiwa kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), kwa kushirikisha taasisi za fedha nchini na wadau wengine kutoka mashirika ya umma.
Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu akielezea kuhusu mkutano huo alisema kuwa kila baada ya miaka miwili taasisi zote za fedha nchini hukutana kuzungumzia maendeleo ya sekta ya fedha na uchumi wa Tanzania kwa ujumla.
Alisema, “Kwa upande wa uchumi safari hii tutajikita katika kuangalia namna gani Tanzania inaweza kutumia fursa zake za kijiografia kukuza uchumi wake.”
Hata hivyo, habari kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa mkutano huo, zilieleza hali ya kiuchumi na kuyumba kwa taasisi ya fedha ni moja ya mambo ambayo yatazungumzwa.
“Hata kama kwenye mada haitakuwepo, lakini ni wazi lazima suala la hali ya uchumi na kudhoofika kwa mitaji ya mabenki tutajadili, ”alisema mmoja wa wadau wa mkutano huo.
Mkutano huo, unakuja wakati baadhi ya taasisi za fedha zikiwapo mabenki, kusitisha kutoa mikopo mipya kwa wateja wao.
Mmoja wa watendaji wa taasisi kubwa ya mikopo jijini hapa, alisema wamepokea maelezo kutoka makao makuu, mapema mwezi huu kusitisha mikopo mipya.
“Kuna hofu ya kupotea kwa fedha kutokana na mikopo hasa baada ya kuyumba kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja, sasa wakubwa wameagiza tusitishe mikopo mipya,” alisema.
Alisema, pia benki kubwa tatu nchini, zimesitisha mikopo mipya ikiwapo ya wafanyakazi kutokana na hali ya uchumi.
Hata hivyo, ilibainika kuyumba kwa mitaji ya mabenki pia kumetokana na uamuzi wa Serikali kuagiza mashirika ya umma kupeleka moja kwa moja fedha BoT badala ya benki binafsi.
“Mkoa wa Arusha umeathirika sana na uamuzi huu, kutokana na mashirika makubwa fedha zake kuhifadhiwa Benki Kuu,”alise
0 Comments