MAUAJI YA VIKONGWE YAITIKISA - SHINYANGA

Kwa ufupi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Muliro Jumanne amesema watu 28 wanaodaiwa kujihusisha na mauaji ya vikongwe tayari wametiwa mbaroni.

Shinyanga. Mkoa wa Shinyanga umeendelea kushuhudia matukio ya mauaji ya vikongwe ambapo kati ya Juni 2015 na Julai, mwaka huu wameuawa 28.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Muliro Jumanne amesema watu 28 wanaodaiwa kujihusisha na mauaji ya vikongwe tayari wametiwa mbaroni.

Amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa baadhi ya wanaojihusisha na mauaji ya vikongwe wanatoka mikoa ya Geita na Tabora na tayari mikakati imeandaliwa kwa kushirikiana mamlaka za mikoa hiyo kuwanasa.

Mkazi wa Manispaa ya Shinyanga,  Mtaa wa Ugweto, Paul Nyanda ameshauri juhudi hizo zihusishe elimu kwa waganga wa jadi ambao ndiyo chanzo cha uchonganisha na kusababisha mauaji ya vikongwe.

Naye Mariam Athuman ameunga mkono hatua za kisheria dhidi ya wanaojihusisha na mauaji hayo huku akishauri jamii ipewe elimu kuhusu madhara ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Kwa miaka mingi, mikoa ya Kanda ya Ziwa imekuw aikishuhudia mauaji ya vikongwe kutokana na imani za kishirikina, jambo ambalo limekuwa likirudisha nyuma maendeleo ya jamii husika

0 Comments