MBUNGE WA ARUSHA MJINI ANUSURIKA KUTEKWA

Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema, Diwani wa Kata ya Sombetini Ally Bananga na Dereva wake Junior Mtatiro wanusurika kutekwa na wanaohisiwa kuwa majambazi waliokuwa wamepanga mawe barabarani usiku wa kuamkia leo, umbali kidogo baada ya kupita Makuyuni kama unaelekea Arusha.

Lema na watu wake walikuwa wakitokea Dodoma kuelekea Arusha ambapo mke wake anasakwa na Polisi kwa kinachodaiwa kuwa amri ya RC, na kukuta majambazi hao wakiwa wameteka Fuso na wamelizibia barabara, ndipo dereva wa Lema akafanikiwa kugeuza gari na kurudi Makuyuni mjini japo walishambuliwa kwa mawe lakini hayakuleta madhara, na ndugu wote  walisalimika.

Pichani, wapo kituo cha Polisi Makuyuni kuomba msaada wa askari ambao walitangulia mbele kuwaescot .

0 Comments