Kwa ufupi
Alisema mfumo wa elimu nchini hauwafanyi watu wajiamini, hivyo amewataka wananchi wazidi kumwomba Mungu awape roho ya kujiamini na kufanya mambo kwa usahihi.
Dar es Salaam. Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam, Valentino Mokiwa amesema changamoto inayolikabili Taifa ni kutojiamini kwa watu wake, jambo linalowafanya waishi kwa wasiwasi.
Alisema mfumo wa elimu nchini hauwafanyi watu wajiamini, hivyo amewataka wananchi wazidi kumwomba Mungu awape roho ya kujiamini na kufanya mambo kwa usahihi.
Askofu Mokiwa alisema hayo jana mjini hapa wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Krismasi, akiomba hofu ya Mungu itawale ndani ya jamii ili watu wasifanye maovu, hivyo amani ya kudumu iwapo.
0 Comments