Jela
Kwa ufupi
Hussein alihukumiwa kifungo hicho jana baada ya Mahakama kuridhishwa na ushahidi wa mashahidi watano.
Dar es Salaam. Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imemhukumu Shaaban Hussein (29), kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kubaka mtoto wa miaka tisa.
Hussein alihukumiwa kifungo hicho jana baada ya Mahakama kuridhishwa na ushahidi wa mashahidi watano.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Catherine Kihoja alisema upande wa mashtaka ulipeleka mashahidi watano ambao walithibitisha shtaka hilo pasipo kuacha shaka yoyote.
Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo Wakili wa Serikali, Neema Moshi aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa mujibu wa sheria kwa sababu mtoto aliyefanyiwa kitendo hicho ameathirika kisaikolojia na alikuwa anatoa harufu mbaya sehemu za siri.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo tarehe isiyofahamika mwezi Julai 2016 eneo la Kipunguni B jijini Dar es Salaam.
0 Comments