SIMULIZI ENDELEVU YA ELIMU TANZANIA

 

Ndugu zangu, 

Mwanazuoni Born Again Pagan ameendelea kusimulia kupitia mtandao.

Kwamba  kufuatia kutangazwa kwa Azimio la Arusha serikali ilitaafisha, kwa manufaa ya umma, nyenzo nyeti za uchumi. Azimio la Arusha lililoungwa mkono na vijana wengi kutembea kwa miguu, kwa mifano, kutoka Arusha hadi Dar es salaam na mmoja wa viongozi wake kufia njiani.

Mwalimu Nyerere pia alitembea kwa miguu kutoka Butiama hadi Mwanza kuwatia nguvu vijana hao kwa kutembea. Vijana wengine walitembea kutoka Bukoba hadi Mwanza kama sio Dar es Salaam na wengine kutoa sehemu za huko kusini (Mbeya na Iringa).

Sambamba na utaifishaji huo, serikali ilibadilisha mkakati wa maendeleo vijijini kwa kuachana na sera za awali za “kunyesha misaada kutoka juu” kupitia “Makazi Mapya” (Rural Village Settlements): Upper Kitete (Arusha), Ikwiriri (Pwani), Luganga (Iringa), na makazi mengine huko Handeni (Tanga).

Lakini mkakati huu, licha ya misaada kemukemu, ulishindikana. Wananchi hawakuwa tayari kuhamia vijijini! Tanzania ikaanza pole pole kuagiza watu wajiunge na Vijiji vya Ujamaa kwa kuanzia huko Mkoa wa Dodoma.

Kukaja  mgogoro wa Mashariki ya Kati uliojikita katika ukombozi wa wa-Palestina kutoka kuwafikiria kuwa ni wakimbizi tu kwenda katika suala la ukombozi wao. Msimamo huo uliingilia uhusiano wetu na serikali ya Israel, hususan, kufuatia vita ya mwaka 1967 ambapo Israel iliteka sehemu ya Afrika ya Sinai (Misri). Tanzania ilivunja uhusiano na Israel.

Hadi kufikia wakati huo, Israel ilikuwa imewekeza katika kuanzisha Jeshi la Kujenga Taifa, misaada mingine ya ki-Jeshi la Ulinzi na usalama, utalii (ikiwa ni pamoja na kutujengea Hoteli za ki-talii, kwa mfano, Kilimanjaro kupitia Kampuni ya Uendeleaji wa ma-Hoteli ya Molonot), biashara ya Karadha, na miradi mingine ya kilimo cha kiangazi (kumwagilia mashamba).

Uhusiano huo ulihusu serikali. Lakini kuna watu walionufaika binafsi, pia. Kwa mfano, Mama Maria Nyerere alipata nafasi ya kwenda huko kusomea Mambo ya Nyumbani (Domestic Science) pamoja na utaalaamu wa kufuga kuku hapo Kigamboni.

 Tanzania ikawa ni kisima cha ma-Profesa wenye mlengo wa kushoto (ma-Soshalisti), kwa mfano, kufuatia mapinduzi ya Ghana, wakaja ma-Prof. David Kimble (Political Science) na mkewe (Uchumi); kutoka Denmark akaja Prof. Knud Svendsen kuwa Profesa wa Uchumi (mshauri wa mambo ya uchumi kwa serikali na chama), Prof. Chodak (Sosiolojia), Prof. Osborn (Fisikia), na Prof. Wellbourne (Elimu).

Wengine walikuwa Prof. Goran Heyden (aliyeondoka na mke wa ki-Haya), na baadhi ya ma-Soshalisti ambao hawakuweza kuhubiri na kutekeleza imani yao makwao (Ulaya/Amerika), kwa mfano. Prof. R. H. Green. Mshauri wa mambo ya Fedha kutoka Chuo Kikuu cha Sussex,Uingereza, na Prof. White (Sheria) aliyeondoka na mke wa ki-Chagga!

Kulikuwepo na ma-Profesa wengine kutoka Visiwa vya Karibe (Caribbeans), kama akina Walter Rodney (Historia) na Earl Carl James (Public Management/Sheria). Hata Jaji KuuBiron alikitokea huko huko Karibe. Wengine walitoka Kenya: Grant Kamenju (Fasihi), Kiara (Sheria) na Lionel Cliffe (Sayansi ya Siasa). 

Hii Ni simulizi endelevu.

0 Comments