TUTAWAFUATA WATOTO WAMITAANI WALIPO - NACTE

Kwa ufupi

Chanzo cha kuwapo kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini ni wazazi kuwafanyia ukatili wa kimwili jambo linalowafanya wazikimbie familia zao.

Dar es Salaam. Mkakati wa kuwahudumia  watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi kuanzia ngazi ya mtaa umeanza kuandaliwa.

Ofisa Maendeleo ya Jamii kutoka Kata ya Kibamba wilayani Ubungo, Fatma  Bangu alisema hayo wakati  wa kutunuku vyeti kwa watoto 42 waliohitimu mafunzo ya ujasiriamali katika Kituo cha Kulelea Watoto cha Spring of Hope.

 Alisema mpango huo utakwenda sanjari na kuwashirikisha wadau mbalimbali pamoja na jamii.

Bangu alisema  chanzo cha kuwapo kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini ni wazazi kuwafanyia ukatili wa kimwili jambo linalowafanya wazikimbie familia zao.

Mkurugenzi wa Huduma ya Utumishi kutoka Shirika la Watawa la Mabinti wa Maria Immakulata (DIM), Vijili Dali alisema waliwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu baada ya kukosa fursa ya kujiendeleza.

Mwenyekiti wa  Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte), Steven Mlote alisema wahitimu hao watakwenda kuwahamasisha wenzao kuwa kuna maisha mapya sehemu nyingine, hivyo wasikate tamaa.

0 Comments