Ndugu zangu,
Kuna simulizi ya Bwana yule mwenye hekima aliyekwenda kwenye mkutano wa Khalifa Haroun Arrashid.
Bwana yule mwenye hekima alikuwa ni mshauri wa Khalifa na mwenye mazoea ya kuhudhuria mikutano ya Khalifa Haroun Arrashid.
Siku moja akiwa kwenye mkutano, Bwana yule mwenye hekima na ambaye aliaminiwa na Khalifa Haroun Arrashid, alimwona Khalifa Arrashid akiwa kwenye mabishano makubwa na wapinzani wake.
Bwana yule akamwambia Khalifa Haroun Arrashid;
" Hivi, ungefanyaje kama ungalikuwa jangwani na ukawa na kiu kali ya maji, akatokea mtu mwenye maji na akakwambia; kuwa yu tayari kukupa maji kwa sharti la wewe kumpa nusu ya mali zako?
Khalifa Haroun Arrashid akajibu;
" Ningekubali"
Bwana yule mshauri wa Khalifa akaongeza;
" Na ungefanyaje kama ungelikuwa mwenye kuhitaji, na kwamba ungepaswa utoe maji yako ili unusurike, lakini hukuweza, na akatokea mtu akakwambia; nipe nusu ya mali yako ili nikusaidie.
Khalifa Haroun Arrashid akajibu;
" Ningefanya hivyo".
Naam, inahusu mambo mawili; ujasiri na unyenyekevu. Kwa mwanadamu, lililo na faida kubwa ni kuwa nayo yote mawili.
0 Comments