LISHE BORA

Unashangaa? Ndio, unaweza kumfanya mwanao awe akili kwa chakula tu! Ndio sababu kuna vyakula vinarutubisha ubongo kuliko vingine,  sasa ukivikazania hivyo utakuta mwanao anakua na akili kuliko wengine wasiokula vyakula hivyo.

Siri iko kwenye kifungua kinywa!
Kibongobongo tunaita chai, ila kwa Kiswahili sanifu ni kifungua kinywa. Hiki wataalam wanasema kazi yake si kufungua kinywa tu, hata ubongo unafunguka. Tafiti zinaonyesha kuwa watoto wanaopata kifungua kinywa wanafanya vizuri kwenye test za kuangalia attention na kumbukumbu, kuliko wale wasiopata kifungua kinywa. Na wote tunajua, attention darasani ndio inamfanya mtoto aelewe, afu kumbukumbu ndio inamfanya afanye vizuri kwenye mtihani au hata application ya vitu alivyojifunza baadae. Hivyo bila hivyo vitu viwili mtoto kufanya vizuri darasani si rahisi.

Kwa nini chai/kifungua kinywa?
Kwa sababu chakula ndio mafuta ya miili yetu, sasa mtoto anamka mafuta yamepungua, inabidi ajaze tumbo ili kila kitu kiende sawa, ni pamoja na uwezo wa akili yake.

Ila sio kila chakula kina matokeo chanya  lakini kitu chochote ni bora kuliko kutokula kabisa, maana watoto wengine wanachagua sana vyakula.

Baadhi ya vyakula vya kurutubisha ubongo:
Peanut butter (siku hizi ziko kibao, mini market yeyote unapata)
Mayai
Ndizi mbivu
MaziwaMtindi
Asali (unaweza kuipaka kwenye mkate)
Hadi hapo tuko sawa.

0 Comments