MITANDAO YA KIJAMII YATOA AJIRA



Mitandao ya kijamii nchini Tanzania imekua kwa kiasi kikubwa.

Kinyume na vijana wengine ambao huitumia mitandao hiyo kuonyesha mambo yasiyofaa, wasichana wawili wahitimu wa Chuo Kikuu wamefanikiwa kujipatia ajira wao pamoja na takriban vijana kumi wengine chini yao.

Leila Athuman na Muse Marwa kupitia ukurasa wao wa Instagram ufahamiakao kama MetalsTanzania wameanzisha kiwanda kidogo ambacho hukitumia kutengeneza bidhaa kama vitanda, viti na bidhaa nyingine za vyuma.

Mwandishi wetu Arnold Kayanda amekitembelea kiwanda chao Mikocheni jijini Dar es Salaam.

0 Comments