MTWARA KUSHIKA MKIA SIYO BAHATI MBAYA


Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego


Kwa ufupi

Mkuu huyo amesema licha ya kutofurahishwa na matokeo hayo, alitarajia hali ingekuwa hivyo kutokana na suala la elimu kutopewa kipaumbele mkoani Mtwara.

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego amesema mkoa huo kutangazwa kushika mkia katika matokeo ya upimaji wa kitaifa wa wanafunzi wa kidato cha pili,  siyo bahati mbaya.

Mkuu huyo amesema licha ya kutofurahishwa na matokeo hayo, alitarajia hali ingekuwa hivyo kutokana na suala la elimu kutopewa kipaumbele mkoani Mtwara.

Amesema tangu ateuliwe kuongoza mkoa huo, amegundua kuwa mambo mengi hayaendi sawa katika elimu, hali iliyomlazimu kujiwekea mikakati ya kujipanga upya.

“Nimekuja Mtwara nimegundua mambo hayako sawa, nikajaribu kutafuta kiini, ndiyo nikabaini hakuna mwamko wa elimu, walimu siyo wabunifu. Wanashindwa kuangalia mazingira yaliyopo na kufundisha kulingana nayo. Utoro pia umekithiri,” amesema.

                                                                    

0 Comments