MWANAFUNZI AFA MAJI GEITA



Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema  mwili huo ulipatikana juzi baada ya jitihada za wavuvi wa eneo hilo kwa kushirikiana na wananchi.

Chato.  Mwili wa mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Sekondari ya Chato mkoani Geita, Shilinde Nicolaus (18) umeopolewa Ziwa Victoria baada ya kuzama Januari 28 saa tisa alasiri alipokuwa akivua na wenzake.

Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema  mwili huo ulipatikana juzi baada ya jitihada za wavuvi wa eneo hilo kwa kushirikiana na wananchi.

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Muungano lilipotokea tukio hilo, Kapembe Charles alisema kijana huyo na wenzake ambao walinusurika, walipata ajali hiyo  baada ya mtumbwi wao kupigwa na dhoruba kisha kuzama.

Charles alisema katika tukio hilo wenzake wawili, Daud Deus na Mgonyolo Hamis wote wakazi wa Kijiji cha Kitela walinusurika  baada ya kuogelea hadi nchi kavu.

Mmoja wa wanafunzi hao, Daud Deus alisema wakati wakiendelea  kuvua, kulikuwa na upepo mkali uliosababisha mtumbwi wao kuzama.

“Mimi na Hamis tulifanikiwa kuogelea kwenye majani yaliyoota ndani ya maji, kisha tukaokolewa na wavuvi,” alisema Deus.

Hata hivyo, Kamanda Mwabulambo alisema wanaendelea kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini undani wa tukio hilo.

0 Comments