Ndugu zangu,
Kuna kisa cha bwana mmoja aliyekuwa akitafuta kazi. Akafika mahali akaona tangazo, kuwa anatafutwa mtu awe simba wa kwenye zoo, mahali pa kuhifadhia wanyama wa kufugwa. Zoo ilikuwa na simba watano, mmoja alikufa, alihitajika mmoja azibe nafasi.
Bwana yule akauliza; "Inakuwaje mniingize kwenye zoo niwe pamoja na simba hawa?!" Akaambiwa;
" We bwana ustie shaka, utavishwa ngozi. Utavalishwa sanamu ya simba. "
Kwamba yeye atakaa juu ya mti tu wakati simba wengine wakiwa chini.
Ikafika siku watalii walikuwa wakiwaangalia simba wale. Akatokea mtalii aliyefanya jambo la kuchekesha sana. Bwana yule akiwa juu ya mti alicheka sana mpaka akaanguka.
Katikati ya simba wale wanne, bwana yule alilia kwa kupaza sauti;
" Jamani eee, niokoeni, mie sio simba, nitaliwa na simba hawa"
Kwa mshangao wa bwana yule, simba wale wakatamka;
" Ewe bwana uwe na amani, sisi pia sio simba, tumevishwa sanamu za simba tu!"
Naam, wanadamu wakati mwingine tumekuwa na hofu ya wanadamu wenzetu hata tukasahau, kuwa wao si simba wala chui. Ni wanadamu kama sisi. Na tunalifahamu hili tunapoanza kuzungumza kama ndugu.
Naam, hii ni zawadi maalum Ya Mwaka Mpya Kutoka Kwa Mwenyekiti Wako. Ni kicheko cha kutafakarisha.
Happy New Year!
0 Comments