Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani
Kwa ufupi
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Tamisemi), Seleman Jafo ametoa agizo hilo alipofanya ziara ya kukagua miundombinu katika shule za msingi za Chadulu, Chang’ombe A na B za Manispaa ya Dodoma.
Dodoma. Serikali imewataka wakuu wa wilaya nchini kuwachukulia hatua kali za kisheria wazazi watakaoshindwa kuwapeleka shule watoto wao.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo ametoa agizo hilo alipofanya ziara ya kukagua miundombinu katika shule za msingi za Chadulu, Chang’ombe A na B za Manispaa ya Dodoma.
Jafo ameema Serikali haitamvumilia mtu atayeshindwa kumpeleka mtoto shule kwa sababu ambazo hazina ukweli
“Hatutaki mtoto akose elimu, mzazi ambaye mtoto wake atabainika hajakwenda shule na kupewa kazi zingine kama kuendesha bodaboda hatua za kisheria zitachukuliwa mara moja,” amesema Jafo.
Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Godwin Kunambi amesema wanaendelea kukabiliana na changamoto, ikiwamo ya ujenzi wa shule za msingi na sekondari.
Ofisa Elimu wa Manispaa hiyo, Scholastika Kapinga amesema hadi jana zaidi ya watoto 8,000 walikwisha kuandikishwa kuanza masomo ya elimu ya awali na msingi.
0 Comments