António Guterres ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Kwa ufupi
Nimejizatiti kujenga na kuanzisha jukwaa la ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na viongozi wa Afrika. Hii ni muhimu katika kusongesha maendeleo jumuishi na kuimarisha ushirikiano kwa ajili ya amani na usalama.
By António Guterres
Ninapoitazama Afrika, naona bara la matumaini, ahadi na fursa nyingi tofauti na dunia ambayo, mara nyingi, huitazama Afrika kupitia kioo cha matatizo.
Nimejizatiti kujenga na kuanzisha jukwaa la ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na viongozi wa Afrika. Hii ni muhimu katika kusongesha maendeleo jumuishi na kuimarisha ushirikiano kwa ajili ya amani na usalama.
Huu ndiyo ujumbe wangu niliouwasilisha hivi karibuni kwenye mkutano wa viongozi wa Muungano wa Afrika huko Addis Ababa, Ethiopia kwenye ziara yangu ya kwanza ya ngazi ya juu nikiwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Ninashawishika kusema, dunia ina mengi ya kunufaika kutoka kwenye busara za Afrika, mawazo na suluhisho.
Afrika inatoa idadi kubwa ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa kote ulimwenguni. Mataifa ya Afrika ni miongoni mwa wenyeji wa idadi kubwa ya wakimbizi na yanaongoza kwa ukarimu. Afrika ndiko kuliko baadhi ya nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi pia.
Azimio la hivi karibuni kuhusu mzozo wa kisiasa nchini Gambia kwa mara nyingine limedhihirisha uthabiti wa Umoja wa Afrika (AU) katika kukabili changamoto za uongozi na kuzingatia demokrasia, haki za binadamu na utawala wa kisheria.
Niliondoka kwenye mkutano wa viongozi wa AU nikiwa nimeshawishika kuwa binadamu wote watanufaika kwa kujifunza na kufanya kazi na Waafrika.
Jamii ya kimataifa kwa mwaka wa pili sasa inatekeleza ajenda ya 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs), ambayo ni juhudi za pamoja kukabili umaskini, usawa, kukosekana kwa utulivu na haki. Afrika imeridhia ajenda yake inayofanana nayo na yenye matarajio makubwa: Ajenda 2063.
Ili Waafrika waweze kunufaika na jitihada hizi muhimu, ajenda hizi mbili zinahitaji kuunganishwa kimkakati.
Dunia yetu inahitaji kuachana na kushughulikia majanga na badala yake kuzuia. Tunahitaji kuepuka urasimu wa kuchelewa kuchukua hatua au kuchukua hatua kidogo kiasi cha kutokidhi haja iliyopo.
Idadi kubwa ya majanga ya zama za sasa ni ya ndani, yakichochewa na kugombea madaraka, rasilimali, ukosefu wa usawa, kuenguliwa kwa baadhi ya makundi na mgawanyiko wa kidini. Mara nyingi huchochewa na misimamo mikali au huwa sababu ya kichocheo.
Umoja wa Mataifa umejizatiti kushirikiana bega kwa bega na wadau wake popote pale kwenye mzozo au tishio la mzozo unaoweza kuhatarisha utulivu na ustawi wa binadamu.
Hata hivyo, kinga ni zaidi ya kuangalia mzozo peke yake. Njia bora zaidi ya kuzuia na kuweka mwelekeo wa uhakika wa amani ya kudumu ni maendeleo endelevu na jumuishi.
Tunaweza kuharakisha maendeleo kwa kuwapatia fursa na matumaini vijana. Zaidi ya wakazi watatu kati ya watano barani Afrika wana umri wa chini ya miaka 35. Kutumia vema kundi hili ina maana kwamba kuwekeza zaidi kwenye elimu, mafunzo, ajira za staha na kujumuisha vijana katika kuandaa mustakabali wao.
Halikadhalika, ni lazima, kwa kadri ya uwezo wetu, tuwawezeshe wanawake kuwa na dhima kamilifu kwenye maendeleo na amani endelevu. Nina furaha kuwa Umoja wa Afrika umekuwa ukilipatia kipaumbele suala la usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake.
Nimeshuhudia hii mara kwa mara. Pindi wanawake wanapowezeshwa, dunia nzima inakuwa imewezeshwa.
Nimesafiri Afrika kama mdau, rafiki na mtetezi aliyejizatiti kubadili simulizi kuhusu bara hili muhimu na lenye mambo tofauti
0 Comments