
Siku ya Jumanne, Januari 31, Dudumizi Technologies alipata wasaa kutoa mafundisho kwa wanasheria wanaosomea mafunzo ya sheria kwa vitendo kwenye shule ya sheria Tanzania (The Law School of Tanzania). Mafundisho hayo yalilenga juu ya njia bora za kutumia ICT kwenye kuongoza taasisi na makampuni ya sheria Tanzania.
Sambamba na matumizi hayo ya ICT, wanasheria hao walipata nafasi ya kujionea programu mpya ambayo ni moja ya product za Dudumiziinayowawezesha kuongeza ufanisi wa ufanyaji kazi zao. Programu hiyo inayoitwa DuLawsiyo tu inawawezesha kuchunga kesi (Case Management), pia inawawezesha kuchunga mafaili, taarifa za mienendo ya kesi, matukio (events), taarifa za kifedha (Invoices), taarifa za wateja, mawasiliano ya wateja na wafanyakazi, kupata ujumbe juu ya taarifa muhimu, kupata repoti juu ya utendaji wa kampuni na mengine mengi.
Programu hii ambayo inapatikana online kwenye tovuti http://dulaw.co.tz unaweza kuitumia popote ulipo kwa kutumia kifaa chochote, iwe simu au kompyuta ya mpakato. DuLawtofauti sana na programu nyingine, ambapo yao imetengenezwa mahususi kwa ajili ya mfumo wa Kisheria wa Tanzania, hivyo, hautakiwi kufanya lolote la ziada kuifanya DuLaw iweze kumanage taarifa zako za kisheria kwa matakwa ya hapa Tanzania.
Dudumizitukiwa moja ya kampuni bora za Website Design hapa Tanzania, tunakuhakikishia usalama na ulizinzi wa bidhaa hii. Dulawinafanyiwa backeup kila siku huku kila akaunti ikitumia njia bora za kuchunga taarifa za kwenye mitandao.
0 Comments