UKATILI WAONGEZEKA

Wakati vitendo vya ukeketaji vikipungua kutoka asilimia 15 hadi asilimia 10 ndani ya miaka mitano, vitendo vya ukatili hasa kwa watoto vinazidi kuongezeka ambapo matukio ya watoto waliofanyiwa ukatili yameongezeka kutoka 2448 mwaka 2014 hadi kufikia 9541 mwaka jana.

Takwimu hizo zimetolewa na kamishna wa Polisi jamii nchini Mussa Ally Mussa wakati akizindua mtambo wa kielektroniki wa ukusanyaji taarifa za ukatili wa kijinsia uliotolewa na jukwaa la watoto CDF kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya kupinga ukeketaji duniani.

Akizungumza katika uzinduzi huo mkurugenzi wa CDF Bw Koshuma Mtengeti amesema mikoa iliyokuwa inatajwa kuongoza kwa takwimu za ukeketaji kwa sasa vitendo hivyo vimepungua ikiwemo Mara na Manyara huku mkuu wa wilaya ya Tarime akielezea namna ambavyo serikali inapambana na mangariba kutokana na wao kubadilisha mbinu za ukeketaji mara kwa mara.

0 Comments