UNDP YAZINDUA VYOO KWENYE SHULE 10 ZA MSINGI - MOSHI


 Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini ,Alvaro Rodriguez pamoja na Mkuu wa wilaya ya Moshi Kippi Warioba wakizindua rasmi vyoo vilivyojengwa katika shule za msingi 10 wilayani Moshi za kufadhiliwa na UNDP.

 Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeelo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alavaro Rodriguez pamoja na Mkuu wa wilaya ya Moshi Kippi Warioba wakitizama vyoo vilivyojengwa na UNDP katika shule ya Msingi Mandela.

 Mkuu wa Idara ya Ushirikino wa Afria Mashariki ,Balozi Celestine Mushy (katikati) akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kippi Warioba (Kulia) kushoto ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya mara baada ya kuzinduliwa kwa vyoo katika shule za msingi za Mandela na Azimio.

  Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeelo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez na ujumbe wake wakiangalia vyoo vya kisasa vilivyojengwa katika shule 10 katika manispaa ya Moshi na Manispaa ya Moshi.

   Jengo la Choo kipya na cha kisasa kilichojengwa katika shule za Msingi  za Azimio na  Mandela vilivyojengwa na UNDP.

 Jengo la Choo cha zamani katika shule ya msingi Azimio. 

 Jengo la Choo cha zamani katika shule ya Msingi Mandela.

 Choo maalumu kwa ajili ya walemavu kilichojengwa katika vyoo vipya vilivyojengwa na UNDP katika shule ya msingi 10 za Msingi wilayani Moshi

 Shimo la Choo cha zamani katika jengo la zamani ,shule ya msingi Mandela.

 Muonekano mpya wa jengo la kisasa la Choo lililojengwa katika shule za Mandela na Azimio

 

Wanafunzi katika shule ya Msingi Mandela wakinawa Mikono katika Choo kipya cha kisasa

 

Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi rasmi wa Vyoo 10 zilizojengwa katika shule za msingi 10 za wilaya ya Moshi.

 

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya akiteta jambo na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeelo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez  wakati wa uzinduzi wa vyoo katika shule za msingi.

 Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeelo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Majengo ya vyoo katika shule 10 za Msingi,Moshi.

  
Mkuu wa Idara ya Ushirikino wa Afria Mashariki ,Balozi Celestine Mushy akizungumza katika uzinduzi huo.

 
Mstahiki Meya wa Mamispaa ya Moshi,Raymond Mboya akizungumza wakati wa uzinduzi huo.

 
Baadhi ya wanafunzi katika shule za Msingi Mandela na Azimio wakiwa katika uzinduzi huo. 

 Wanafunzi katika shule za Msingi za Azimio na Mandela wakitoa burudani za nyimbo na Ngoma wakati wa uzinduzi rasmi wa Vyoo katika shule za msingi za Azimio na Mandela.

 Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini ,Alvaro Rodriguez wakiwa katika picha za pamoja na viongozi wengine pamoja na kamati ya shule hizo.

Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini ,Alvaro Rodriguez wakiwa katika picha za pamoja na wanafunzi wa shule za Azimio na Mandela.

*************

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Mwakiishi wa Shirika la Mipango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania ,Alvaro Rodriguez,akishirikiana na Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Balozi Celestine Mushy wamezindua vyoo 10 vilivyojengwa katika shule za msingi 10 wilayani Moshi.

Ujenzi huo ulifanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya uwapo wa Umoja wa Mataifa.

Wakati wa maadhimisho hayo pia wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa walifanya shughuli mbalimbali mkoani Kilimanjaro za kusaidia maendeleo ikiwamo hifadhi ya mazingira na usafi.

Katika kuhakikisha kwamba shule zinakuwa na UNDP Tanzania ilisaidia mkoa wa Kilimanjaro  Sh Mil 510 kujenga vyoo vya kisasa katika shule za msingi 10 ili kusaidia kuezesha usafi kwa wanafunzi na walimu wao.

Hadi kufikia sasa jumla ya matundu 178 yamejengwa katika shule 10 ambapo matundu 104 ni kwa ajili ya wasichana na 74 kwa ajili ya wavulana.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mwakilishi makzi wa UNDP.Alvaro Rodriguez alipongeza mradi huo na ushirikiano uliokuwepo kati ya serikali ,wao na shule ikiwa ni hatua moja ya maendeleo endelevu kwa kuboresha mazingira ya usafi kwa wanafunzi wa kike na wa kiume katika masomo yao na hivyo kuimarisha safari ya kuelekea malengo ya dunia ya 2030.

Alisema kutokuwepo kwa mazingirabora ya usafi ni chanagamoto kubwa kwa wanafunzi na hali hiyo inawaathiri sana wanafunzi wa kike.

Rodriguez alisema kutokana na kujengwa kwa vyoo hivyo wanafunzi ,walimu na walezi sasa watakuwa na kazi pekee ya kuhakikisha kwamba wanatoa elimu bora .

“Watoto wa kike watakuwa na changamoto chache zaidi za mahudhurio shuleni na wakati huo huo masUala ya usafi yatakuwa yameboreka na hivyo kuwa na wanafunzi na familia zenye siha njema.”alisema Rodriguez.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Balozi Celestine Mushy amepongeza kwa msaada huo na kuutaka Umja wa MAtaifa kuendelea kutoa msaada kwa shule zenye mahitaji makubwa kuhakikisha kwamba malengo ya dunia yanayohusiaa na usafi ,mazingira na maji safi yanafanikiwa ifikapo mwak 2030.

Naye mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba pamoja n kuishukuru UNDP kwa kazi nzuri waliyofanya pia alizitaka jumuiya za maeneo yaliyojengewa vyoo kuiliki msaada huo kwa kuhakikisha wanaitumia na hivyo kuisadia kufikia malengo ya dunia 2010.

0 Comments