GRACA MACHEL AZINDUA MPANGO WA KUWAINUA WANAWAKE AFRIKA


Mke wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Graca Machel amesema mapinduzi  yanayotakiwa kufanyika hapa nchini kwa sasa ni ya kuwainua wanawake kiuchumi, kiafya na kijamii.

Mama Machel, ambaye ni mke wa Hayati Nelson Mandela amesema hayo leo Ijumaa wakati wa mkutano na wanahabari alipozindua mpango wa kuwainua wanawake Afrika."Mapinduzi ya kwanza yalifanikiwa wakati ule tunatafuta uhuru lakini,"amesema.

Mama Machel amesema wanawake hawana budi kushika usukani katika kuhakikisha wanafanikiwa kiuchumi na katika sekta zote za maendeleo.

Kwa upande wake Mwanzilishi wa Tanzania Women Chambers, Anjelina Maleko amesema kama wanawake wamebarikiwa kwa jambo moja hawana budi kuwa baraka kwa wenzao.

Mke wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Graca Machel akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa kuhusu changamoto wanazozipata wanawake kiuchumi na katika sekta zote za maendeleo wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuwainua wanawake Afrika uliofanyika katika leo jijini Dar es Salaam.

Rais wa VoWET na Mkurugenzi Mtendaji wa IBRA Construction Limited Bi. Maida Waziri akiongea akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchango wa Mke wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini mama Graca Machel alivyomsaidia kufikia malengo hasa kwenye suala la elimu.

Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC), Jacqueline Mneney Maleko akizungumzia mafanikio yake pamoja na njia wanazoweza kuzitumia wanawake ili kufikia malengo waliyojiwekea.

Baadhi ya waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa waliofika kwenye uzinduzi wa  mpango wa kuwainua wanawake Afrika na Tanzania ikiwa nchi ya kwanza.

Mke wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Graca Machel(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa VoWET na Mkurugenzi Mtendaji wa IBRA Construction Limited Bi. Maida Waziri(kushoto) 

Mke wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Graca Machel akizungumza na mmoja waadishi wa habari mara baada ya kufanyika uzinduzi wa uzinduzi wa  mpango wa kuwainua wanawake Afrika.

0 Comments