Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene
Kwa ufupi
Simbachawene alisema baadhi ya watendaji wasiokuwa waaminifu kwa makusudi, wamesitisha ajira za baadhi ya watumishi wenzao kwa kutumia mgongo wa uhakiki wa vyeti.
Dar es Salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amewataka watumishi wa umma waliositishiwa ajira zao kimakosa wakati wa uhakiki wa vyeti wapeleke vielelezo vyao Tamisemi.
Simbachawene aliyasema hayo jana Jijini Arusha alipokuwaakifungua Mkutano Mkuu wa Tisa wa wadau wa mfuko wa pensheni wa LAPF.
Simbachawene alisema baadhi ya watendaji wasiokuwa waaminifu kwa makusudi, wamesitisha ajira za baadhi ya watumishi wenzao kwa kutumia mgongo wa uhakiki wa vyeti.
Alitoa rai kwa watumishi hao kufika haraka kwenye ofisi za Tamisemi wakiwa na nyaraka zitakazosaidia kuwarejesha kazini.
“Kuna baadhi ya watendaji waliokuwa wakifanya uhakiki wa vyeti vya wafanyakazi hawakutenda haki, yao walionewa katika uhakiki huo, hivyo nawaomba wafike ofisi za Tamisemi wakiwa na vielelezo vyao,” alisema Simbachawene.
0 Comments