SHEHE wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajab amesema moja ya majukumu makubwa ya wazazi ni kuwalea watoto katika maadili ili wawe na tija kwa taifa.
Sheikh Rajabu ambaye pia ni Kadhi wa Mkoa alisema hayo wakati akizungumza na akinamama wa Kiislamu katika Sherehe za Maulidi ziliyofanyika kwenye Uwanja wa Punda wilayani Kondoa mkoani Dodoma.
Alisema wazazi na walezi wanao wajibu kuwalea watoto katika misingi ya maadili badala la jukumu hilo kuiachwa kwa serikali na taasisi nyingine za malezi zikiwamo dini na shule.
Alisema tabia ya baadhi ya wazazi kutoshiriki kikamilifu malezi ya watoto, inaongeza mmomonyoko wa maadili na ongezeko na vitendo viovu katika jamii vinavyowakosesha watoto mwelekeo wa kimaisha.
Mkurugenzi wa Kituo cha Alhaafidhu Islamic Orphan Centre Kondoa Ukh-ti, Aisha Nobbe alisema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya kukosekana kwa chakula cha kutosha.
Alisema kituo kina watoto zaidi ya 300 ambao ni yatima na wanaoishi katika Mazingira magumu kutoka mikoa mbalimbali na kituo hicho hakina ubaguzi wa kiitikadi, kiimani, kabila wala rangi.
0 Comments