MTOTO ASIMULIA ALIVYOBAKWA NA WATU WATANO

Wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspapers (TSN) Ltd wakiwa kwenye maandamano ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa katika Viwanja vya Mwembe Yanga Tandika, Dar es Salaam jana. (Picha na Yusuf Badi).

WAKAZI wa Kibaha mkoani Pwani, wamebubujikwa machozi baada ya mtoto wa miaka 14 (jina linahifadhiwa), kueleza jinsi alivyobakwa na watu watano, huku kukiwa hakuna hatua madhubuti zilizochukuliwa kwa wabakaji hao.

Hayo yalijitokeza mjini Kibaha wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, ambayo iliandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake mkoani Pwani (PWMO).

Wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo, ambayo yalifanyika kwenye Uwanja wa Bwawani Maili Moja, walionekana wakilia wakati akitoa ushuhuda wa jinsi alivyobakwa. Akisimulia, mtoto huyo alisema alibakwa na watu watano. Tukio hilo lilitokea mwaka jana.

Mtoto huyo alikuwa akisoma darasa la saba. Tukio hilo lilimuathiri kisaikolojia. Alisema siku ya tukio alikuwa ametumwa dukani na njiani akakutana na kijana, akamshika kwa nguvu na kumvutia vichakani, ambaye alianza kumwingilia na ghafla wakatokea wengine wanne.

Yule wa kwanza alipomaliza, akaanza wa pili na wakati huo wote alikuwa akipiga kelele. Kelele hizo zilisababisha vijana hao kukimbia na kumwachia majeraha na maumivu makali. Alieleza kuwa kesi hiyo ilipelekwa mahakamani, lakini imekuwa ikisuasua, hivyo kuleta hofu kuwa haki inaweza isipatikane.

Awali, akiibua suala hilo la ubakaji, Diwani wa Viti Maalumu, Elina Mgonja alisema vitendo vya ukatili kwa wanawake ikiwemo ubakaji, vimekithiri huku wanawake na watoto wakikosa haki zao na kunyanyaswa. Mgonja alisema baadhi ya watu, wamekuwa wakifumbia macho vitendo hivyo vya unyanyasaji 

0 Comments